Imam Khomeini alihuisha Uislamu na kuwapa Waislamu utambulisho
(last modified Wed, 09 Feb 2022 04:32:04 GMT )
Feb 09, 2022 04:32 UTC
  • Imam Khomeini alihuisha Uislamu na kuwapa Waislamu utambulisho

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran amesema hayati Imam Khomeini- Mwenyezi Mungu Amrehemu, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alihuisha Uislamu na kuwapa Waislamu utambulisho

Manouchehr Mottaki aliyasema hayo Jumanne mjini Tehran wakati akihutubu katika kongamano la kimataifa la “Mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Mapambano (Muqawama) Duniani.”

Mottaki amesema ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu ni sawa na ule wa Mtume Muhammad SAW nao ni kubadilisha mtazamo wa mwanadamu kuhusu dunia.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iran amesema maisha ni medani ya mapambano ya daima na kukabiliana na uwongo. Ameendelea kusema kuwa Imam Khomeini alikuja kuhuisha mapambano hayo. Aidha Mottaki amesema Imam Khomeini alikuja na ujumbe mpya wa kuasisi ustaarabu mpya.

Manouchehr Mottaki

Hivi sasa wananchi wa Iran wamo katika maadhimisho ya Alfajiri Kumi kuelekea kilele cha shehere za kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran tarehe 22 Bahman sawa na tarehe 11 Februari.

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi mwaka 1979 kwa uopngozi wa Imam Ruhullah Khomeini na yameendelea kupata nguvu na kuwa na ushawishi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni licha ya njama za madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani.