Qalibaf: Marekani ingali inafuatilia sera za ubeberu dhidi ya Iran
(last modified Wed, 17 Aug 2022 12:27:03 GMT )
Aug 17, 2022 12:27 UTC
  • Qalibaf: Marekani ingali inafuatilia sera za ubeberu dhidi ya Iran

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Marekani ya leo, ndiyo ile ile ya huko nyuma ya wakati wa mapinduzi ya serikali Iran ya mwaka 1953 (Mapinduzi ya Mordad 28).

Mohammad Baqer Qalibaf amesema hayo leo Jumatano katika kikao cha Bunge kilichofanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kurejea hapa nchini kundi la kwanza la mateka wa kivita raia wa Iran kutoka Iraq mnamo Agosti 17, 1990, na kuogeza kuwa: Kiwango na kina cha mtazamo wa kibeberu wa Washington mkabala wa nchi nyingine ikiwemo Iran, hakijabadilika hata kidogo.

Amebainisha kuwa, Mapinduzi ya 1953 ni moja ya mifano ya wazi na isiyopingika inayoonesha kuwa madola ya kibeberu hayajali chochote kuhusu demokrasia na uhuru.

Qalibaf amefafanua zaidi kwa kusema,  "Dola la kibeberu linapoona kuwa linapoteza maslahi yake, huwa linadhalilisha na kudunisha uhuru wa kujitawala nchi nyingine.'

US na Ugaidi

Ameeleza bayana kuwa, dunia inapaswa kuungana katika kupambana na siasa za kibeberu za Marekani, za kupenda makuu na kujikumbizia kila kitu upande wake.

Spika wa Bunge la Iran ameeleza kuwa, Ikulu ya White House ya Marekani ndio muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Kizayuni, ambao ndio mzizi na chimbuko la jinai na maafsa katika eneo la Asia Magharibi. 

Ameongeza kwa kusema, Marekani iliyapa silaha makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq kwa shabaha ya kuvuruga usalama na mamlaka ya kujitawala mataifa ya eneo kama Iran.

Tags