Iran: Kombe la Dunia limeonesha namna utawala wa Kizayuni unavyochukiwa na walimwengu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91156-iran_kombe_la_dunia_limeonesha_namna_utawala_wa_kizayuni_unavyochukiwa_na_walimwengu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unachukiwa na mataifa mengi ya dunia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 30, 2022 13:00 UTC
  • Iran: Kombe la Dunia limeonesha namna utawala wa Kizayuni unavyochukiwa na walimwengu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unachukiwa na mataifa mengi ya dunia.

Nasser Kanaani amesema hayo katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter leo Jumatano na kueleza kuwa, hatua ya baadhi ya madola ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel haijawafanya wananchi wa nchi za Kiarabu waache kuuchukia utawala huo wa Kizayuni.

Kanaani ameeleza bayana kuwa, Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar limekuwa jukwaa la walimwengu kuonesha ni jinsi gani wanauchukia utawala haramu wa kibaguzi wa Israel.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran amesema mashindano hayo makubwa zaidi ya kandanda duniani yanayoendelea nchini Qatar yametumiwa pia kutangaza uungaji mkono na mshikamano na wananchi wa Palestina.

Watazamaji kutoka Qatar, Tunisia, Lebanon na hata Saudi Arabia wamekataa kuhojiwa na waandishi wa habari wa Israel. Waaandishi wa utawala wa Kizayuni wamesusiwa kikamilifu na wanashindwa kufanya mahojiano na watu, kwani kila wanapojitambulisha kuwa ni kutoka Israel, Waarabu wanawakwepa kama ukoma huku wengine wakisema waziwazi kuwa katika dunia hakuna kitu kinachoitwa Israel. 

Kombe la Dunia la Qatar; Jukwaa la kutangaza mshikamano na Wapalestina

Siku chache zilizopita pia, mwandishi mmoja Mzayuni, Ben Hamo, ambaye anaelewa vizuri lugha ya Kiarabu na ni Mzayuni mwenye chuki ambaye anajigamba waziwazi kuwa yeye ni Mzayuni, alisema waziwazi kuwa, tusijidanganye, Waarabu hawaupendi kabisa utawala wa Kizayuni.

Akthari ya wanachi wa nchi za Kiarabu wamekuwa wakifanya maandamano ya kulalamikia kitendo cha watawala wa nchi zao cha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel.