Jan 02, 2023 07:41 UTC
  • Raia wa nchi nne walihusika katika mauaji ya Kamanda Qassem Soleimani

Mkuu wa kamati maalumu ya ufuatiliaji wa kisheria na wa kimataifa wa faili la mauaji ya Kamanda Qassem Soleimani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, raia wa nchi nne walihusika katika mauaji ya kamanda huyo.

Abbas Ali Kadkhodaei, ameliambia shirika la habari la ISNA kuwa, "katika hati ya mashtaka iliyoandaliwa kuhusu kesi hii, kwa upande wa washtakiwa, yametajwa majina ya raia wa nchi kadhaa kwamba ndio wahalifu na wasimamizi katika utekelezaji wa mauaji hayo".
Kadkhodaei ameongezea kwa kusema: Katika uga wa kisiasa na diplomasia ya umma pia, imebainishwa jinsi kesi hii itakavyowasilishwa na kufuatiliwa katika jumuiya za kimataifa na mbele ya fikra za waliowengi.
Mkuu wa kamati maalum ya ufuatiliaji wa kisheria na kimataifa wa mauaji ya Hajj Qassem Soleimani amebainisha pia: "tuna njia kadhaa tunazoweza kuzitumia katika jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kuwafuatilia wale waliotenda jinai hii isiyosameheka".
Kadkhodaei amesema: katika uga wa kisheria, ombi lililoandaliwa kuhusiana na kesi hii karibu litakamilika, na tunaweza kufuatilia suala hili kulingana na mamlaka tuliyo nayo kwa mahakama za ndani kuhusiana na jambo hili.
Mkuu huyo wa kamati maalumu ya ufuatiliaji wa kisheria na kimataifa wa mauaji ya Hajj Qassem Soleimani amesisitiza kwa kusema: raia watano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliuawa shahidi katika jinai ya uwanja wa ndege wa Baghdad, na kwa kuzingatia Kanuni ya Adhabu ya Kiislamu, tunayo mamlaka ya kufungua kesi ndani ya nchi kuhusiana na jinai iliyotokea .../

 

Tags