Abdollahian: Iran inasaidia kupatikana amani na uthabiti barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93538-abdollahian_iran_inasaidia_kupatikana_amani_na_uthabiti_barani_afrika
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ipo mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi na inasadia kupatikana amani na uthabiti barani Afrika.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Feb 01, 2023 04:06 UTC
  • Abdollahian: Iran inasaidia kupatikana amani na uthabiti barani Afrika

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ipo mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi na inasadia kupatikana amani na uthabiti barani Afrika.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo mbele ya waandishi wa habari nchini Mauritania baada ya mazungumzo yake na Rais wa nchi hiyo Mohamed Ahmed Ould Ghazouni na kusisitiza kwamba, Tehran imekuwa ikitoa kipaumbele katika sera zake za kigeni juu ya kukuza na kuimarisha uhusiano na mataifa ya Kiafrika.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza juhudi zenye thamani za Rais Mohamed Ahmed Ould Ghazouni wa Mauritania katika kufuatilia ubunifu wa kupambana na ugaidi na kuimarisha amani na uthabiti wa kudumu katika eneo la Sahara Magharibi na kubainisha kwamba, Tehran inaunga mkono uthabiti wa kiuslama wa bara la Afrika na vilevile kupatikana dunia yenye amani na utulivu.

Aidha kabla ya hapo na katika mazungumzo yake na Rais wa Mauritania na maafisa wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo akiwemo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo, Abdollahian alijadili na kubadilishana nao mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya uhusiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa ikiwemo kadhia ya Palestina sambamba na kustawishwa zaidi uhusiano baina ya mataifa ya Kiislamu.

Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yupo nchini Mauritania katikak safari rasmi ya kikkazi ambapo anauongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kidiplomasia na kisiasa wa Iran katika safari hiyo.