Balozi wa Kenya Tehran atembelea kiwanda cha kutengeneza matrekta nchini
(last modified Tue, 14 Mar 2023 07:58:40 GMT )
Mar 14, 2023 07:58 UTC
  • Balozi wa Kenya Tehran atembelea kiwanda cha kutengeneza matrekta nchini

Balozi wa Kenya mjini Tehran ametembelea kiwanda cha uzalishaji matrekta nchini Iran na kueleza kuwa, Kenya inataraji kutumia zana na mashine za kilimo kwa ajili ya ustawi na uendelezaji wa sekta hiyo.

Kampuni ya Traktor-Sazi nchini Iran kwa sasa ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa zana na matrekta ya kilimo ikiwa ni mashirika tanzu 12 katika mji wa Tabriz, mashirika 2 nje ya mkoa wa Azerbaijan Magharibi na mashirika mawili nje ya mipaka ya Iran.  

Kundi hilo la viwanda mwaka huu limetengeneza zaidi ya matrekta elfu 31; na kuuza matrekta 2,500 katika nchi zaidi ya 20 kwa thamani ya dola milioni 45.   

Kiwanda cha kuzalisha matrekta cha mjini Tabriz, Iran 

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Joshua Gatimu Aguta Balozi wa Kenya nchini Iran amesema pambizoni kwa ziara yake ya kulitembelea kiwanda hicho cha uzalishaji matrekta huko Tabriz kuwa: uzalishaji wa trekta hapa nchini unaendana zaidi na mahitaji ya kilimo ya Kenya.

Balozi wa Kenya hapa nchini, Joshua Gatimu Aguta amewaalika viongozi wa Kampuni hiyo ya uundaji matrekta kushiriki katika maonyesho yajayo ya kilimo huko Kenya ili kutangaza zaidi uzalishaji unaofanywa na kampuni hiyo. 

Mustafa Vahedzadeh Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la viwanda la uzalishaji wa matrekta la Iran pia amesema katika ziara hiyo kuwa, Kampuni ya Traktor-Sazi iko tayari kushirikiana katika nyanya zote ili kustawisha mfumo wa sekta ya kilimo huko Kenya na kueleza kuwa Traktor-Sazi inaweza kufungua njia ya uzalishaji na uuzaji bidhaa huko Kenya kama njia mbadala iliyoko mezani.  

Vahedzadeh ameongeza kuwa, matrekta yanayotengenezwa Iran hivi sasa yanatumika mashambani kwa ajili ya shughuli za kilimo katika nchi zaidi ya 25 duniani.