Mar 16, 2023 10:49 UTC
  • Kana'ani: Mkakati wa Iraq kuzipatanisha Iran, Saudia mzizi wake ni Soleimani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria mapatano ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia na kueleza kuwa, msingi wa jitihada za Iraq za kuzipatanisha Tehran na Riyadh unatokana na mitazamo ya kistratajia ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Nasser Kan'ani amesema hayo katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa Twitter leo Alkhamisi na kueleza kuwa: Shahidi Soleimani hakuwa tu shujaa katika mapambano dhidi ya ugaidi, lakini pia alikuwa 'msanifu majengo' katika masuala ya amani, maridhiano na udugu baina mataifa na nchi za Kiislamu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza byana kuwa, Jenerali Soleimani alifahamu na kutambua asili na njama za maadui, kwa kuwa alikuwa na maono ya mbali.

Kana'ani amesisitiza kuwa, chimbuko na mzizi wa Iraq wa kuwa mpatanishi baina ya Iran na Saudia ni Shahidi Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Makubaliano baina ya Iran na Saudia yaliafikiwa Ijumaa iliyopita ya Machi 11 katika mji mkuu wa China, Beijing, baada ya siku kadhaa za mazungumzo magumu kati ya Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran (SNSC) Ali Shamkhani na mwenzake wa Saudia.

Saudi Arabia ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Iran mnamo Januari 2016 baada ya waandamanaji wa Iran, waliokasirishwa na hatua ya Saudia kumyonga ngozi mashuhuri wa Kishia Sheikh Nimr kuvamia ubalozi wake mjini Tehran na ubalozi mdogo wa Riyadh mjini Mash'had.

Tags