Raisi: Mustakbali unatia matumaini kwa kambi ya mapambano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i96092-raisi_mustakbali_unatia_matumaini_kwa_kambi_ya_mapambano
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Jamhuri ya Syria kwamba mustakbali unaonekana kuwa mzuri na wenye kuleta matumaini kwa harakati ya muqawama na mapambano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2023 23:17 UTC
  • Raisi: Mustakbali unatia matumaini kwa kambi ya mapambano

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Jamhuri ya Syria kwamba mustakbali unaonekana kuwa mzuri na wenye kuleta matumaini kwa harakati ya muqawama na mapambano.

Katika mazungumzo hayo ya simu na Rais Bashar Assad wa Syria, Rais wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, amempongeza kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kusema kuwa, mfumo wa dunia unabadilika kwa maslahi ya mhimili wa mapambano na dhidi ya mfumo wa kibeberu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema: Jinai za utawala huo ni ishara ya udhaifu na kukata tamaa kwake, na ni uthibitisho wa mustakbali mzuri na wenye matumaini kwa harakati ya mapambano.

Akigusia matukio yanayojiri katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, Rais Ebrahim Raisi ameongeza kuwa: "Jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni ni ishara ya udhaifu na uthibitisho wa mustakbali mzuri na wenye matumaini wa harakati ya muqawama."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza haja ya kuheshimiwa ardhi yote ya Syria na kusema kuwa njia pekee ya kupambana na ugaidi ni kuunga mkono mamlaka ya kitaifa ya Syria.

Kwa upande wake Bashar Assad, Rais wa Syria, amelipongeza taifa la Iran kwa mnasaba wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Rais Assad ameashiria miongo minne ya mapambano ya Iran na Syria dhidi ya maadui wa pamoja na kusema: Leo hii dalili za kuporomoka zinaonekana waziwazi katika jamii ya Kizayuni na haya ni matunda ya mapambano na kusimama kidete hususan taifa la Palestina.