Apr 22, 2023 02:31 UTC
  • Rais wa Iran awatumia Waislamu salamu za pongezi kwa mnasaba wa  Sikukuu ya Idul-Fitr

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za kheri na fanaka kwa Waislamu kwa mnasaba wa kuwadia siku kuu ya Idul Fitr ambayo ni siku ya kurejea katika Fitra na ni wakati wa fahari na furaha kwa waliofunga katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na waja wema wa Mwenyezi Mungu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ebrahim Raisi  amewapongeza viongozi na wananchi wa nchi za Kiislamu na Waislamu kote dunaini kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idul Fitr. Katika ujumbe wake, Rais wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa, kwa baraka za Idi hii adhimu na pia kwa kufungamana na mafundisho makubwa ya Uislamu na mafundisho yenye kuleta uhai ya Mtume Muhammad SAW, kutashuhudiwa  kuongezeka umoja na mshikamano wa Umma wa Kiislamu na kuimarika ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu ili kwa njia hiyo malengo yenye kuleta uhai ya Uislamu yaweze kufikiwa.

Kwa mujibu wa tangazo la Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo Jumamosi ni tarehe Mosi Shawwal na hivyo ni siku kuu ya Idul Fitr.

Katika baadhi ya nchi nyingine za Kiislamu, zikiwemo Iraq, Oman na Pakistan, Indonesia, Malaysia, Moroko na Brunei, leo ni Idul Fitr. Aidha Saudi Arabia, Bahrain, Qatar, Syria, UAE na Uturuki, Misri, Kuwait, Yemen, Palestina, Lebanon na Jordan zilitangaza Ijumaa kuwa siku ya kwanza ya Shawwal na siku ya Idul Fitr.

Tags