Jun 07, 2023 10:24 UTC
  • Rais wa Iran kutembelea Venezuela, Nicaragua na Cuba

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni atafanya ziara katika nchi tatu za Venezuela, Nicaragua na Cuba kwa lengo la kuimarisha uhusiano na nchi rafiki na kupanua kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kisayansi na nchi hizo.

Viongozi wa Iran na wa nchi tatu za Venezuela, Nicaragua na Cuba watasaini hati kadhaa za ushirikiano katika nyanja mbalimbali katika ziara hiyo ya Jumapili ijayo ya Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko  Amerika ya Latini kwa ajili ya kuimarisha kiwango cha uhusiano na ushirikiano na nchi hizo tajwa.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha atakutana na kuzungumza na wafanyabiashara na wanaharakati wa masuala ya uchumi wa ndani na wa Kiirani huko Venezuela, Nicaragua na Cuba.

Nchi kadhaa za eneo la Amerika ya Latin mbali na uwezo mbalimbli wa kiuchumi zilionao, zina mitatazamo ya kisiasa na kimataifa inayokaribiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Iran na nchi hizo unaweza kuleta manufaa mengi kwa pande zote mbili.

Tags