Jul 17, 2023 04:33 UTC
  • Gharib Abadi: Haki itatekelezwa katika kuwashughulikia wahusika wa mauaji ya Shahidi Soleimani.

Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Iran amesisitiza kuwa uadilfu utatendeka katika kuwashughulikia wahusika wa mauaji ya Shahidi kamanda Soleimani.

Luteni Jenerali Haji Qassim Soleimani, Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq ya Al Hashdu Shaabi na wanajihadi wengine kadhaa waliuawa Januari Tatu 2020 katika shambulio la anga la vikosi vamizi na vya kigaidi vya Marekani katika uwanja wa ndege wa Bagdhad mji mku uwa Iraq.  

Abu Mahdi al Muhandes (kushoto) na Haj Qassem Soleimani 

Kazem Gharib Abadi Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mchakato wa sasa wa faili la shahidi Kamanda Qassim Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes na kusema: Kitendo cha Marekani cha kuwaua kigaidi mashahidi hawa ni jinai dhidi ya binadamu na akasema: Haki itatendeka katika kuwashughulikia wahusika wa mauaji ya Shahidi Soleimani. 

Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu pia ameongeza kusema kuwa: "Wamagharibi wanafanya juhudi kuutwisha ulimwengu mtindo wao wa maisha bila ya kuzingatia aina za tamaduni." Amesema, "mienendo ya undumakuwili na kuziainishia sheria nchi nyingine kuhusu haki za binadamu kuna madhara makubwa katika uwanja huo na sisi tunapinga jambo hilo."  

Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu amesema: Iran na Iraq ni wahanga wa vikwazo na mauaji ya kigaidi. Huko Iraq watoto laki tano wasio na hatia wameuliwa ikiwa ni natija ya vikwazo vya Marekani na Magharibi. 

Gharib Abadi ameongeza kuwa: Maelfu ya watu wamekuwa wahanga wa ugaidi nchini Iraq na Iran; na wahusika wa jinai hizo ni makundi ya kigaidi yaliyoasisiwa na nchi zinazodai kutetea haki za binadamu.  

Tags