-
Araqchi atahadharisha kuhusu njozi za "Israel Kubwa" kabla ya mkutano wa dharura wa OIC
Aug 24, 2025 08:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ametahadharisha kuwa kuwepo njozi za "Israel Kubwa" kunawakilisha hatari na tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia. Araqchi amezitolea wito nchi za Kiislamu kuchukua hatua za pamoja kukabiliana na ajenda ya kujitanua ya Israel.
-
IRGC: Uhusiano wa kina kati ya serikali, wananchi na vikosi vya ulinzi ni dhamana ya Iran yenye nguvu
Aug 24, 2025 07:25Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeashiria umuhimu wa uhusiano wa kina uliopo kati ya serikali, taifa na vikosi vya ulinzi likiutaja kuwa muhimu kwa ajili ya kuwa na nchi yenye nguvu na iliyoendelea. Jeshi la IRGC aidha limesisitiza dhamira yake ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi na usalama kwa kuzingatia vitisho vilivyopo.
-
Rais Pezeshkian aipongeza timu ya astronomia ya Iran kwa kushinda ubingwa wa dunia
Aug 24, 2025 04:34Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameipongeza Timu ya Olimpiadi ya Astronomia ya Iran kwa kushinda taji la ubingwa wa dunia kwa mwaka wa pili mfululizo.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa magaidi waliokuwa na silaha za Marekani
Aug 23, 2025 23:28Maafisa wa usalama nchini Iran wamefanikiwa kusambaratisha mtandao wa kigaidi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa nchi, karibu na mpaka wa Pakistan, na kuwaua magaidi sita huku wakikamata wawili.
-
Najafi: Iran na IAEA zimefanya mazungumzo ya upigaji 'hatua mbele' kuhusu mfumo mpya wa ushirikiano
Aug 23, 2025 07:30Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema, pande hizo mbili zimefanya mazungumzo ya upigaji 'hatua mbele' kuhusu namna ya kuratibu mfumo mpya wa ushirikiano kati yao.
-
Iran: Tutatumia zana mpya iwapo adui ataanzisha tena uchokozi
Aug 23, 2025 03:33Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesisitiza kuwa, iwapo maadui watafanya uchokozi mwingine dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, bila shaka majeshi ya nchi hii yatatumia vifaa, silaha na zana za kijeshi ambazo hazijawahi kutumiwa kufikia sasa.
-
Iran yaionya Ulaya juu ya matokeo mabaya ya kuamilisha 'snapback'
Aug 23, 2025 02:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ameionya Ulaya juu ya matokeo mabaya ya kuamilisha "utaratibu wa snapback", akisisitiza kwamba Troika ya Ulaya (Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani) pamoja na Umoja wa Ulaya hazina haki ya kisheria na ya kimaadili ya kutumia utaratibu huo.
-
Larijani: Wamagharibi watambue kuwa Iran haiogopi vita
Aug 23, 2025 00:52Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Larijani, amethibitisha tena dhamira ya Tehran kushiriki katika mazungumzo ya kidiplomasia huku akionya kwamba mazungumzo ya maana yanaweza kusonga mbele tu endapo Marekani na Ulaya zitakubali kuwa mashinikizo na vitisho vya vita haviwezi kuwatisha wananchi wa Iran.
-
Mkuu wa Jeshi: Iran itatoa 'jibu kali la kusagasaga zaidi' kwa uchokozi wowote mpya wa adui
Aug 22, 2025 08:20Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu Iran Meja Jenerali Amir Hatami amesisitiza kuwa Vikosi vya Ulinzi vimejiweka tayari kutoa jibu kwa wavamizi ambalo ni la "kusagasaga zaidi" kuliko lile lililoonekana wakati wa uchokozi uliofanywa na utawala haramu wa kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Ziara ya Pezeshkian Yerevan na Minsk; Kufafanuliwa tena nafasi ya Iran katika mfumo mpya wa Eurasia
Aug 22, 2025 04:31Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezzekian, katika nchi za Armenia na Belarus, wanachama wawili wa Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia ni lengo la Tehran la kuendeleza uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na nchi za eneo hilo na zile za Caucasus Kusini.