Iran
  • Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia

    Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia

    Sep 06, 2025 03:31

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa liidhinishe juhudi za kidiplomasia katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa Tehran na kukomesha vitendo vya "kinyume na sheria" vya Ulaya.

  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa

    Sep 05, 2025 23:36

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".

  • "Hatua ya nchi za Ulaya kuamilisha utaratibu wa snapback ni ya kiholela"

    Sep 05, 2025 08:38

    Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswalia leo hapa Tehran amesema: Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, jaribio lolote la kubadilisha Azimio Nambari 2231 linadhoofisha itibari ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuamilisha utaratibu wa "snapback" wa kurejesha vikwazo vya baraza hilo dhidi ya Iran ni ya kiholela.

  • IRGC: Adui hana ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran

    IRGC: Adui hana ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran

    Sep 05, 2025 07:33

    Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema Israel na washirika wake hawana uwezo wala ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran, hivyo basi, wamekimbilia operesheni za vita vya kisaikolojia.

  • Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia

    Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia

    Sep 05, 2025 07:32

    Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amesema Marekani na utawala wa Israel zilifanya mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya vituo vya nyuklia ya Iran, licha ya vituo hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nyuklia.

  • Araqchi: 'Iran itaendelea kuunga mkono Muqawama wa Palestina dhidi ya Israel'

    Araqchi: 'Iran itaendelea kuunga mkono Muqawama wa Palestina dhidi ya Israel'

    Sep 05, 2025 03:37

    Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesisitiza dhamira ya nchi hiyo ya kuunga mkono Muqawama halali na mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel hadi pale haki zao zitakaporejeshwa kikamilifu.

  • Ripoti: Takriban Wairani 100 walikuwa wahanga wa ugaidi katika mwaka uliopita wa Kiajemi

    Ripoti: Takriban Wairani 100 walikuwa wahanga wa ugaidi katika mwaka uliopita wa Kiajemi

    Sep 04, 2025 22:52

    Mashambulizi ya kigaidi yaligharimu maisha ya takriban Wairani mia moja katika mwaka uliopita wa kalenda ya Kiirani, uliomalizika Machi 20. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali linalowakilisha familia za wahanga Wairani wa mashambulizi ya kigaidi.

  • Araqchi: IAEA imeafiki haja ya mfumo mpya wa ushirikiano na Iran

    Araqchi: IAEA imeafiki haja ya mfumo mpya wa ushirikiano na Iran

    Sep 04, 2025 22:49

    Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa hakutakuwa na ushirikiano mpya baina ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hadi hapo mazungumzo yatakapokamilika.

  • Iran yalipiza kisasi: Balozi wa Australia aondoka Tehran

    Iran yalipiza kisasi: Balozi wa Australia aondoka Tehran

    Sep 04, 2025 11:12

    Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametangaza kwamba balozi wa Australia mjini Tehran ameondoka nchini na kuongeza kuwa: "Kwa mujibu wa kaida na sheria za kidiplomasia, katika kukabiliana na hatua ya Australia ya kumfukuza balozi wa Iran mjini Canbera, Jamhuri ya Kiislamu imejibu mapigo kwa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia wa Australia nchini Iran."