-
Iravani: Hakuna mazungumzo na Marekani iwapo nchi hiyo inataka kuitwisha Iran sera zake
Jun 30, 2025 04:29Saeid Iravani Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mazungumzo yoyote hayatawezekana na Marekani chini ya mashinikizo na kwa kuilaizmisha Iran sera zake.
-
Iran yalitaka Baraza la Usalama la UN kuzitambua Israel na Marekani kama pande zilizoanzisha uchokozi
Jun 30, 2025 04:16Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liutambue utawala wa Israel na Marekani kuwa pande zilizoanzisha vita vya karibuni vya siku 12 dhidi ya Jamburi ya Kiislamu ya Iran.
-
Maulamaa Wakuu wa Iran: Shambulio lolote dhidi ya Kiongozi Muadhamu ni jinai ya kivita
Jun 30, 2025 02:29Maulamaa wakuu wa Kiislamu nchini Iran wamesema kuwa shambulio lolote au tishio dhidi ya Kiongozi Muadhamu na Marjai ni sawa na kutenda jinai ya kivita.
-
Je, Iran imekabiliana vipi na bwabwaja za Trump dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi?
Jun 30, 2025 02:16Bwabwaja na hambarara za Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Imam Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa viongozi wa Iran.
-
Jenerali Mkuu: Iran inatilia shaka kufungamana Israel na usitishaji vita
Jun 30, 2025 00:56Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu dhamira ya Israel kutekeleza usitishaji mapigano wa upande mmoja uliotangazwa na Marekani, na akaonya kuwa Iran iko tayari kujibu kwa nguvu kubwa iwapo utawala huo utarejelea uchokozi wake.
-
Spika wa Bunge la Iran alaani kauli za Trump dhidi ya Iran asena ni za za kipuuzi na zisizo na maana
Jun 30, 2025 00:55Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amelaani vikali lugha ya matusi ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kusema kuwa matamshi hayo ni juhudi za bure za kutaka kuhujumu mchakato wa maamuzi ndani ya mfumo wa uongozi wa Iran.
-
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu ahimiza utayarifu wa taifa dhidi ya vitisho vya adui
Jun 29, 2025 11:10Admiral Ali Shamkhani, mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesisitiza ulazima wa kuwa macho na kuwa tayari kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya maadui, huku akitaka kustawishwa zaidi uwezo wa kijeshi wa taifa hili.
-
Rafael Grossi: Iran haina silaha za nyuklia
Jun 29, 2025 08:29Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema kuwa suluhisho la muda mrefu la suala la nyuklia la Iran ni mazungumzo ya kidiplomasia, akisisitiza kuwa Iran haina silaha za nyuklia.
-
Je, mahudhurio ya mamilioni ya watu katika mazishi ya "Mashahidi wa Nguvu" yametoa ujumbe gani kwa walimwengu?
Jun 29, 2025 08:25Mazishi ya "Mashahidi wa Nguvu" ya Iran yamekuwa dhihirisho la mshikamano na uzalendo wa Wairani wa matabaka tofauti, ambao wametuma ujumbe wa umoja wao wa kitaifa kwa walimwengu kupitia ushiriki wao mkubwa katika mazishi hayo.
-
Baqaei: Matakwa ya Wairani ya haki na uadilifu hayatafifia
Jun 29, 2025 04:35Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, matakwa ya Wairani ya ukweli na uadilifu hayatafifia, kwa sababu jinai za kivita na jinai dhidi ya ubinadamu hazitapitwa na wakati.