-
Pezeshkian amjibu Trump: Inaonekana huwajui kabisa Wairani
May 15, 2025 04:09Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amejibu kauli za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Iran na kusema kuwa, inaonekiana kiongozi huyo wa Marekani hawafahamu wananchi wa Iran.
-
Spika Qalibaf: Maendeleo ya ulimwengu wa Kiislamu yanategemea ushirikiano wa Iran na Saudi Arabia
May 15, 2025 04:08Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuwepo umoja baina ya nchi za Kiislamu na kubainisha kwamba, Iran na Saudi Arabia zinapaswa kutumia fursa iliyojitokeza kuendeleza uhusiano wao sambamba na maendeleo ya Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran ina wajibu wa kusimama dhidi ya tawala kandamizi
May 15, 2025 01:10Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema lazima Iran isimame dhidi ya tawala zinazoua watoto pamoja na wale wanaowaunga mkono na kusitisha ukandamizaji, na itaendelea kufanya hivyo licha ya uadui unaoibuliwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran kuishtaki "Google" kwa kupotosha jina la "Ghuba ya Uajemi"
May 15, 2025 00:35Kituo cha Kitaifa cha Anga za Juu cha Iran kimesema kitachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Google ya Marekani na majukwaa mengine ya kimataifa kutokana na kupotoshwa kwa jina la kihistoria la Ghuba ya Uajemi.
-
Qalibaf ataka ushirikiano wa vikwazo dhidi ya Israel na kuundwa nchi huru ya Palestina
May 14, 2025 08:09Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezitaka nchi za Kiislamu kuuwekea vikwazo vya kisiasa, kiuchumi na kijeshi utawala wa Kizayuni wa Israel ili kukomesha mauaji ya kimbari huko Gaza.
-
IRGC yajibu vitisho vya US: Iran ipo tayari kwa senario yoyote
May 14, 2025 08:02Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Iran iko tayari kwa hali yoyote ile, wakati huu ambapo Marekani inatoa vitisho vya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya nchi hii, akisisitiza kwamba maadui watafedheheshwa wakijaribu kuingia katika makabiliano na Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran: Hakuna haja ya kuendelea na mazungumzo iwapo Marekani....
May 14, 2025 08:00Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi amesisitiza kuwa haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya kurutubisha madini ya urani ni "mstari mwekundu" wa taifa hili, akisisitiza kuwa, kufikiwa makubaliano na Marekani kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa nchi hii kunategemea kufuata kanuni hizo.
-
Qalibaf: Umoja wa Mabunge ya Asia ni fursa ya kuendeleza uhusiano na nchi za Kiislamu
May 14, 2025 03:28Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amezungumzia umuhimu wa Umoja wa Mabunge ya Kiislamu kwa ajili ya kustawisha uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na kusema: Kushiriki nchi 38 za Kiislamu katika mkutano wa 19 wa Mabunge ya Kiislamu ni fursa ya kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo.
-
Baqaei: Kusimamisha miradi ya nyuklia ya Iran kimsingi si jambo linalojadiliwa katika mazungumzo na Marekani
May 14, 2025 03:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa suala la kusimamisha miradi ya nyuklia ya Iran kimsingi halijadiliwi katika mazungumzo na Marekani na kwamba miradi yetu ya nyuklia bila shaka itaendelea kwa jadi.
-
Iran yailaani Israel kwa kupiga mabomu kambi za wakimbizi Palestina
May 13, 2025 23:17Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mashambulizi ya hivi karibuni ya anga dhidi ya kambi za wakimbizi wa Kipalestina yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel na kusababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya Wapalestina wasio na hatia wakiwemo watoto wadogo.