-
Araghchi: Mzingiro wa bandari za Iran ni uvunjaji wa makubaliano ya usitishaji vita
Apr 23, 2026 10:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ametoa tamko kufuatia shambulio la Marekani dhidi ya meli ya kibiashara ya Iran katika Bahari ya Oman, akisema kwamba kuweka mzingiro dhidi ya bandari za Iran ni uvunjaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Baqaei: Iran Iko tayari kujilinda mkabala wa vitisho vya adui
Apr 23, 2026 09:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza utayari wa Tehran kujilinda dhidi ya mashambulizi na vitisho vya aina yoyote vya adui.
-
Araqchi: Mashambulizi dhidi ya Iran ni chanzo cha ukosefu wa usalama katika Ghuba ya Uajemi
Apr 23, 2026 09:35Mwakilishi Maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, ambaye aliwasili Tehran kwa ajili ya mashauriano na viongozi wa Iran, amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
-
Kiongozi Muadhamu awashukuru Maulamaa wa Kisunni wa Hormozgan
Apr 21, 2026 09:19Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, ameelezea shukrani zake za dhati kwa wanazuoni na maulamaa wa Kisunni katika mkoa wa kusini mwa Iran wa Hormozgan, akisifu mshikamano wao na tamko lao la kutoa Bay’a yaani kiapo cha utii.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vitisho vipya vya Trump dhidi ya Iran
Apr 21, 2026 09:11Msemaji wa Umoja wa Mataifa amekosoa wazi vitisho vipya vya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu kushambulia miundombinu ya Iran endapo matakwa ya Washington hayatatekelezwa.
-
Qalibaf: Hakuna mazungumzo chini ya vitisho, Iran iko tayari kufichua kadi mpya uwanjani
Apr 21, 2026 08:51Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema Tehran haitakubali kufanya mazungumzo na Washington chini ya kivuli cha vitisho.
-
Siku ya Jeshi: Kiongozi apongeza jeshi la Iran kwa ujasiri katika kulilinda taifa dhidi ya wavamizi
Apr 19, 2026 10:57Katika ujumbe alioutoa Jumapili kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei amelisifu Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusimama kwa ujasiri kulilinda taifa katika vita vya hivi karibuni vya kulazimishwa, kama lilivyofanya katika vita vya kulazimishwa vya awamu zilizopita.
-
Iran kudhibiti trafiki ya Lango Bahari la Hormuz hadi makubaliano yafikiwe kumaliza vita
Apr 19, 2026 10:50Baraza la Juu la Usalama wa Taifa la Iran (SNSC) limesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kusimamia na kudhibiti trafiki yote inayopita katika Lango Bahari la Hormuz, ambalo ni njia ya kimkakati, hadi kufikiwa mapatano kamili ya kumaliza vita vya kulazimishwa vya Marekani na Israel dhidi ya nchi hii.
-
Esmaeil Baqaei: Iran yasema haitakubali ubabe wa Marekani katika mazungumzo
Apr 16, 2026 06:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesisitiza kuwa Iran ilikataa mapendekezo aliyoyaita “yasiyo na mantiki” yaliyowasilishwa na Marekani katika mazungumzo yaliyofanyika Islamabad, akionya kuwa Tehran haitawahi kukubali mazungumzo yanayoendeshwa kwa mfumo wa ubabe na kulazimisha masharti.
-
Iravani: Silaha zilizotumiwa katika uvamizi dhidi ya Iran zilitoka kwenye maghala ya baadhi ya nchi za Kiarabu
Apr 15, 2026 08:08Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amepinga madai ya Bahrain, akisema: Mabaki yaliyopatikana kutoka kwenye silaha zilizotumiwa katika mashambulizi ya miji ya Iran yanathibitisha kuwa silaha hizo zilitoka kwenye maghala ya baadhi ya nchi za kiarabu za Ghuba ya Uajemi.