-
Qalibaf: Iran haipingi mazungumzo, inataka diplomasia ichukue mkondo wake
Jan 29, 2026 23:42Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Tehran haipingi msingi wa mazungumzo na diplomasia ambao lazima uwe wa aina yake na wenye mlingano kwa mujibu wa kuheshimiana pande mbili.
-
Iran na Saudia katika mkondo wa ushirikiano na matarajio ya kuleta usalama, ustawi na umoja baina ya Waislamu
Jan 29, 2026 23:17Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman na kusisitiza kwamba: muelekeo inaofuata Iran katika uga wa kikanda umejengwa juu ya msingi wa udugu wa Kiislamu, kustawisha uhusiano wa kirafiki, na kupanua mashirikiano na nchi za Kiislamu.
-
Droni 1,000 za kimkakati zakabidhiwa kwa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jan 29, 2026 09:55Ndege elfu moja zisizo na rubani za kimkakati zimejiunga na vikosi vinne vya jeshi kwa amri ya Meja Jenerali Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
'Ni rahisi - Trump ameshindwa': Wanamtandao wakosoa vitisho vya kijeshi vya Marekani dhidi ya Iran
Jan 29, 2026 09:35Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa vitisho vya kijeshi vya mara kwa mara vya Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya Iran, ambapo hivi karibuni alitishia Iran kwa kisingizio cha miradi ya nyuklia ya nchi hiyo. Wamesema kuwa Israel inaiburuta Washington katika vita vingine kwa niaba ya serikali ya Tel Aviv.
-
IRGC: Iran haitaanzisha vita, lakini ndiyo itakayoamua vitakavyoisha
Jan 29, 2026 03:49Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema Iran ndiyo inayoshikilia mpini na nafasi ya juu katika kuamua hatima ya vita vyovyote tarajiwa, likisisitiza kwamba kutumia mashinikizo ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu hakujazaa matunda.
-
Araghchi: Mazungumzo hayawezi kufanikiwa chini ya vitisho
Jan 29, 2026 00:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi ameonya kwamba, kutwisha diplomasia kupitia vitisho vya kijeshi hakuwezi kuwa na ufanisi au tija, akisema kwamba hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na Tehran kufikia juu ya kufanya mazungumzo na Marekani.
-
Iran: Maadui wajiandae kwa 'jibu la uharibifu' wakituchokoza
Jan 29, 2026 00:18Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran ameonya kwamba, hatua yoyote ghalati dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu itawasababishia maadui uharibifu mkubwa, akisisitiza kwamba vitisho dhidi ya Tehran kupitia maonyesho ya kijeshi havilishughulisha taifa hili.
-
Mtaalamu wa kijeshi: Utitiri wa droni za Iran ni 'tishio halisi' kwa vyombo vya majini vya Marekani
Jan 28, 2026 07:02Mtaalamu wa kijeshi wa ndege zisizo na rubani ameonya kuwa, utitiri wa ndege zisizo na rubani za Iran ni "tishio halisi" kwa vyombo vya jeshi la wanamaji la Marekani vyenye thamani kubwa, wakati huu ambapo Washington inaripotiwa kuwa inaendelea kujizatiti kijeshi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Iran ilivyofanikiwa kuvunja mtandao wa mawasiliano ya kigaidi kwa kukata intaneti
Jan 28, 2026 04:30Iran ilifanikiwa kuvuruga na hatimaye kuvunja mtandao wa mawasiliano wa makundi ya kigaidi na washirika wao wa nje kwa hatua ya kukata intaneti wakati wa machafuko ya Januari 2026.
-
Waziri wa Usalama: Umoja wa kitaifa utazuia vitisho kwa umoja wa kitaifa wa Iran
Jan 28, 2026 04:28Waziri wa Usalama wa Iran amesema kuwa taifa la Iran halitaruhusu umoja wa kitaifa wa nchi hii udhoofishwe akisisitiza kuwa umoja wa taifa la Iran ndiyo nguzo kuu ya kukabiliana na vitisho vya nje.