-
Qalibaf: Maigizo ya Marekani Hormuz yanaweza kusababisha mgogoro mpya wa kifedha duniani
May 15, 2026 09:45Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge), Mohammad-Baqer Qalibaf, ameonya kuwa juhudi za Marekani za kuendeleza mvutano wa kijeshi karibu na Mlango Bahari wa Hormuz zinaweza kusababisha mgogoro mpya wa kifedha duniani, wakati ambapo deni la taifa la Marekani tayari limefikia kiwango kikubwa cha dola trilioni 39.
-
Satelaiti tatu za Iran kurushwa katika anga za mbali karibuni
May 15, 2026 09:33Shirika la Anga za Mbali la Iran (ISA) limetangaza kwamba satelaiti tatu zilizotengenezwa ndani ya nchi zimeingia katika hatua ya mwisho ya majaribio, ishara kwamba mpango wa anga wa kiraia wa nchi hii unastawi kwa kasi licha ya mashinikizo kutoka nchi za Magharibi na utawala wa Kizayuni.
-
Pezeshkian: Mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya viwanja vya michezo yafichua uadui kwa heshima ya Iran
May 15, 2026 06:06Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa kulengwa kwa viwanja vya michezo na miundombinu ya umma na Marekani pamoja na Israel wakati wa vita vya uchokozi kumefichua uadui wa washambuliaji hao dhidi ya heshima, furaha na fahari ya taifa la Iran.
-
Araghchi: UAE ni “mshirika hai” katika uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran
May 15, 2026 06:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, ameikosoa vikali Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuwa mshirika wa moja kwa moja katika uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran. Ametoa kauli hiyo akijibu madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na mwakilishi wa UAE.
-
Araqchi katika mkutano wa BRICS New Delhi: Ushawishi wa Marekani unapungua
May 14, 2026 10:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi amesema kuwa wananchi wa Iran "wamesimama kidete na kwa fahari " dhidi ya machafuko ya kutisha, na kamwe hawatasalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani nchi ambayo ushawishi wake duniani unazidi kupungua.
-
Vyombo vya Habari vya Marekani: Iran bado ina uwezo mkubwa wa makombora
May 14, 2026 08:43Kinyume na madai ya maafisa wa serikali ya Marekani wanaochochea vita, akiwemo Rais Donald Trump, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti, vikinukuu tathmini za siri, kwamba Iran bado ina uwezo mkubwa wa makombora.
-
Jeshi la Iran: Hakuna silaha za Marekani zikazovuka Mlango-Bahari wa Hormuz
May 14, 2026 03:35Jeshi la Iran limetangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu tena silaha za Marekani kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz na kuingia katika vituo vya nchi za kanda hii. Limesema kuwa njia hiyo ya kistratejia ya majini sasa iko chini ya udhibiti wa kimkakati wa vikosi vya ulinzi vya Iran.
-
Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Uko Imara Zaidi ya Ulivyokuwa Huko Nyuma
May 13, 2026 13:11Waziri Mkuu wa zamani wa Qatar ameeleza katika mahojiano marefu aliyofanyiwa na televisheni ya Al Jazeera kwamba, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uko mara zaidi hivi sasa kuliko ulivyokuwa huko nyuma.
-
Wizara ya Ulinzi wa Iran: Kubalini haki za Iran au mkabiliwe na kipigo kingine cha kijeshi
May 13, 2026 12:21Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema maadui, Marekani na Uzayuni, wanapaswa kukubali haki halali za taifa la Iran, au wasubiri kushindwa tena katika nyanja za kidiplomasia na katika uwanja wa vita.
-
Kushiriki UAE katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni 'haramu kabisa'
May 13, 2026 12:18Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa kimetangaza kuwa ushiriki, uwezeshaji na ushirikiano wa UAE katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Iran ni sawa na "kusaidia kambi ya ukafiri dhidi ya ndugu Waislamu" na hivyo, "kimsingi ni haramu."