-
Amir Saeed Iravani: Kamwe Iran haitasalimu amri mbele ya vitisho
Nov 15, 2025 08:57Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Tehran kamwe haitasalimu amri mbele ya vitisho vya kijeshi, mashinikizo ya kisiasa, au vikwazo vya kiuchumi.
-
Qalibaf: Israel haijawahi kuonja moto kama wa Vita vya Siku 12
Nov 14, 2025 23:07Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kwamba: Israel ilikumbaa na mashinikizo makubwa ya kukabiliana na mashambulizi ya Iran hususan katika siku za mwisho za Vita vya Siku 12 na haijawahi kupata kipigo kama ilichopata wakati wa vita vya siku 12 ilivyovianzisha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Jenerali Hassanzadeh: Mifumo ya ulinzi wa dunia inagwaya mbele ya makombora ya Iran
Nov 14, 2025 23:07Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) mjini Tehran, amezungumzia nguvu zinazozidi kuongezeka za Jamhuri ya Kiislamu za kupambna na madola ya kibeberu duniani na kusema: "Katika vita vya siku 12, mifumo jumuishi ya ulinzi ya kimataifa iligwaya na kuzipigia magoti nguvu za makombora za Iran na adui alihisi kushindwa vitani katika muda usiozidi saa 24.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa Tehran: Vyombo vya kidiplomasia vimfungulie mashtaka Trump mhalifu katika majukwaa ya kimataifa
Nov 14, 2025 07:44Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema vyombo vya kidiplomasia vinapaswa kumfungulia mashtaka Donald Trump mhalifu katika majukwaa ya kimataifa.
-
Iran na Uturuki zatilia mkazo kupunguzwa mivutano na kurejeshwa amani na uthabiti katika eneo
Nov 14, 2025 04:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyidd Abbas Araqchi, amefanya mazunguzmo kwa njia ya simu na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan, ambapo wawili hao wamejadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya kikanda na kimataifa.
-
Iran yapinga na kuyatoa maanani madai ya kundi la G7 dhidi yake
Nov 13, 2025 23:52Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, madai yaliyomo kwenye taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazounda G7 uliofanyika nchini Canada kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayana msingi wala nadhari na hayakubaliki.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa mamluki wa Marekani na Israel
Nov 13, 2025 03:51Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kimesambaratisha mtandao wa kijasusi hapa nchini uliokuwa ukiendesha harakati za kuvuruga usalama na amani.
-
Aragchi: UN ichukue hatua baada ya Trump kukiri jukumu katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
Nov 12, 2025 23:34Katika barua rasmi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Abbas Araghchi amelaani Marekani kwa jukumu lake katika kuunga mkono uchokozi wa kijeshi wa Israeli dhidi ya Iran mnamo Juni, kufuatia kauli za Rais Donald Trump akithibitisha usimamizi wa Marekani juu ya mashambulizi hayo.
-
Larijani: Hakuna ujumbe mpya uliotumwa Marekani
Nov 12, 2025 04:08Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amepuuzilia mbali ripoti kwamba kumekuwepo mawasiliano mapya kati ya Tehran na Washington na kusisitiza kuwa hakuna ujumbe mpya uliowasilishwa kwa Marekani.
-
Bandari ya Chabahar ya Iran kuwa lango la chai na kahawa ya Kenya kuelekea masoko ya Asia ya Kati
Nov 11, 2025 23:10Kenya inatazamia kutumia uwezo wa bandari ya Chabahar ya Iran na kama kitovu cha kanda kwa ajili ya uagizaji na usambazaji wa chai na kahawa.