-
Meja Jenerali Abdullahi: Uwezo wa makombora wa Iran ni zaidi ya mawazo ya adui
Mar 08, 2026 09:23Meja Jenerali Ali Abdullahi, amesema majeshi ya ulinzi ya Iran yamejitayarisha kikamilifu kuendeleza mapambano dhidi ya adui na kwamba adui atapata jibu la makosa yake uwanjani na kwenye medani ya vita.
-
Siku ya tisa ya vita; Iran yaendeleza mawimbi ya makombora na ndege zisizo na rubani
Mar 08, 2026 06:23Katika siku ya tisa ya uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alfajiri ya leo limetangaza kutekelezwa kwa mawimbi mapya ya Operesheni ya kulipiza kisasi ya ‘Ahadi ya Kweli 4’
-
Majasusi wa US: Haiyumkiniki kubadilisha mfumo wa uongozi Iran
Mar 08, 2026 04:13Baraza la Ujasusi la Marekani limesema katika tathmini yake 'ya siri' kwamba, ni muhali kubadilisha mfumo uliokita mizizi wa kisiasa na kiusalama nchini Iran, hata kwa kutumia mashambulizi makali ya kijeshi yanayoendelea ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Msemaji wa IRGC: Tunavisubiri kwa hamu kubwa vikosi vya US kwenye Lango-Bahari la Hormuz
Mar 07, 2026 14:18Msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ya Khaatamul-Anbiyaa amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha na kusubiri kwa hamu kubwa kuthibiti kwa madai ya vikosi vya jeshi la Marekani vya kusindikiza meli za mafuta na kujikita kwenye Lango-Bahari la Hormuz.
-
Iran: UN inabeba dhima ya kisheria na kimaadili ya vita haramu vya US, Israel
Mar 07, 2026 10:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei amejibu taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye bila kulaani uvamizi na mashambulizi ya kichokozi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, ameeleza wasiwasi wake juu ya vita hivyo kwa uchumi wa dunia.
-
Maulamaa wa Kishia na Kisunni, wa ndani na nje ya Iran watoa fatua ya Jihadi dhidi ya Marekani na utawala wa kizayuni
Mar 07, 2026 08:37Maraajii Taqlidi wa madhehebu ya Shia, ndani na nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na Maulamaa wakubwa wa Kisunni wa hapa nchini na katika mataifa mengine ya Ulimwengu wa Kiislamu wametoa fatua ya Jihadi dhidi ya Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel kufuatia uchokozi wa kidhalimu walioanzisha dhidi ya ardhi ya Iran.
-
Mazungumzo ya simu kati ya Vladimir Putin na Masoud Pezeshkian
Mar 07, 2026 04:07Rais wa Russia, Vladimir Putin, amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo, ambapo Rais wa Iran amesisitiza kuwa: “ Njia yetu ni kujihami kwa nguvu ili kulinda mipaka yetu na kuleta amani endelevu.
-
Siku ya 7 ya Vita; Vikosi vya Iran Vyalenga Kitovu cha Tel Aviv
Mar 06, 2026 12:29Katika siku ya saba ya vita vya kukabiliana na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza wimbi la ishirini na moja la Operesheni “Ahadi ya Kweli 4”, likihusisha mashambulizi ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni), pamoja na kurushwa kwa makombora ya Kheibar yenye vichwa vingi vya kivita dhidi ya malengo yaliyoko katikati ya Tel Aviv.
-
Pezeshkian: Iran imesimama kidete katika kujihami, kulinda heshima ya taifa
Mar 06, 2026 10:28Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu haitasita kuendelea kujihami na kujilinda mkabala wa mashambulizi ya kichokozi ya maadui wa taifa hili.
-
Araqchi: Yoyote anayeendeleza vita atakwama kwenye kinamasi
Mar 06, 2026 09:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mahojiano yake na mwandishi habari Tom Llamas wa televisheni ya NBC kwamba: Serikali ya Marekani inahusika kikamilifu na umwagaji damu unaoshuhudiwa hivi sasa.