-
Russia yalaani 'uharamia' wa Marekani wa kukamata meli yake ya mafuta
Jan 08, 2026 02:58Moscow imelaani vikali kitendo cha Marekani cha kukamata meli ya mafuta yenye bendera ya Russia katika Bahari ya Atlantic, na kuitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Sheria ya Bahari.
-
Vyama vya Tunisia vyamjia juu Trump kwa kukiuka sheria za kimataifa
Jan 08, 2026 02:39Vyama vya kisiasa na harakati za kijamii na kiraia nchini Tunisia zimetangaza kupinga vikali ajenda ya sera ya kigeni ya Rais wa Marekani Donald Trump, hasa uingiliaji wake wa masuala ya ndani ya Venezuela na ushupaliaji wake wa kutaka kuidhibiti Greenland.
-
Mwanachuoni Nigeria: Israel itafutwa katika uso wa dunia ikiishambulia tena Iran
Jan 08, 2026 02:38Mwanachuoni mashuhuri wa Kiislamu wa kaskazini mashariki mwa Nigeria amezionya Israel na Marekani dhidi ya kufanya mashambulizi yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran, akisema matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi kuliko yale ya vita vya siku 12 vya mwezi Juni mwaka uliopita 2025, na kuilazimisha Israel kuomba usitishaji vita.
-
Iran: Uingiliaji wa Marekani wakusudia kuchochea vurugu na ugaidi
Jan 07, 2026 23:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu Iran imekemea vikali kauli za kuingilia na za upotoshaji zilizotolewa na maafisa wa Marekani kuhusu hali za ndani ya Iran, ikisema matamshi hayo yanaakisi uhasama wa kudumu wa Washington dhidi ya taifa hili na yamelenga kuibua machafuko na hali ya kutokuwa na usalama nchini.
-
Marekani 'yaziwekea ngumu' nchi zingine 12 za Afrika kupata viza ya kuingia nchini humo
Jan 07, 2026 23:36Serikali ya Marekani imeongeza karibu mara tatu idadi ya nchi ambazo wamiliki wa pasipoti zao watahitajika kuweka dhamana ya hadi dola 15,000 ili kuomba kuingia nchini humo.
-
UN yaitaka Israel ikomeshe 'mfumo wa ubaguzi wa apathaidi' inaoendesha Ukingo wa Magharibi
Jan 07, 2026 23:35Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu umesema, hatua za miongo kadhaa za Israel za kuwatenga na kuwabagua Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi inaoukalia kwa mabavu zinazidi kuongezeka, na kwa sababu hiyo umetoa wito wa kuutaka utawala huo ukomeshe "mfumo wake wa ubaguzi wa rangi wa apathaidi".
-
White House: Chaguo la kijeshi kwa ajili ya kuitwaa Greenland lipo mezani
Jan 07, 2026 23:34Ikulu ya White House ya Marekani imesema Rais Donald Trump wa nchi hiyo na washauri wake wanatathmini "machaguo mbali mbali" katika jitihada za kulitwaa eneo la Greenland, likiwemo chaguo la kutumia jeshi la nchi hiyo.
-
UAE yatuhumiwa tena na Saudia; mara hii ni kuwaunga mkono Wadruze ili kuigawanya Syria
Jan 07, 2026 23:33Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa, Saudi Arabia imetoa tuhuma zisizo za kawaida dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu, Imarati huku kukiwa tayari kuna mvutano unaoongezeka kati ya mataifa hayo mawili ya Ghuba ya Uajemi, tuhuma ambazo zinahusu wasiwasi kuhusu namna UAE inavyojihusisha na masuala ya Syria.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel huko Somaliland; Tel Aviv katika njia ya kuyumbisha amani Pembe ya Afrika
Jan 07, 2026 23:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amefanya safari huko Hargeisa, mji mkuu wa eneo la Somaliland, akiongoza ujumbe rasmi wa Israel.
-
Mkuu wa zamani wa Sera za Nje wa EU: Ulaya iache kuifanya Marekani muitifaki wake mkuu
Jan 07, 2026 11:30Josep Borrell, mwanadiplomasia mkuu wa zamani wa Umoja wa Ulaya (EU) amesema, kambi hiyo inapaswa iache kuichukulia Marekani kama mshirika wake mkuu, huku Washington na Brussels zikiwa zinazozana hivi sasa kuhusu sera za kidijitali na udhibiti wa eneo la Greenland.