-
Wabunge wa Uganda watilia shaka uamuzi wa serikali kutaka kupeleka wanajeshi Ghaza
Aug 07, 2026 12:27Baadhi ya wabunge wa upinzani nchini Uganda wametilia shaka uamuzi wa serikali wa kutaka kupeleka wanajeshi wa nchi hiyo huko Ukanda wa Ghaza watakaokuwa sehemu ya kikosi cha kimataifa cha kurejesha uthabiti katika eneo hilo la ardhi ya Palestina.
-
Katika kumbukumbu ya mwaka wa 81 tangu US ilipoishambulia Hiroshima, UN yataka silaha za nyuklia ziangamizwe
Aug 07, 2026 12:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya kuwa dunia inakabiliwa na ongezeko la hatari ya matumizi ya silaha za nyuklia kutokana na kushamiri migawanyiko ya kisiasa, kutokuaminiana na mashindano ya kijeshi.
-
Watetezi wa Palestina washinda katika uteuzi wa wagombea wa Democratic wa uchaguzi wa US
Aug 07, 2026 12:24Matokeo ya uchaguzi wa mashinani wa Marekani wa kuteua wagombea wa Seneti na Baraza la Wawakilishi katika uchaguzi wa Novemba yanaonyesha ushawishi unaoongezeka wa mrengo wa chama cha Democratic unaotaka mabadiliko, ambao umeliweka suala la Palestina kwenye kitovu cha wito wake wa kisiasa.
-
Spika Qalibaf: Mkakati wa Marekani wa vitisho na kuvunja ahadi umefeli
Aug 07, 2026 03:38Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, amekosoa miamala ya hivi karibuni ya Washington kama “diplomasia ya maigizo” isiyo na mashiko, akitangaza kuwa mkakati wa Marekani wa vitisho, kuvunja ahadi, na kusuka simulizi za uongo umefeli. Aidha amesisitiza kwamba Iran haitashiriki katika michezo hiyo ya kuigiza tena.
-
Waziri wa Ulinzi: Vikosi vya Iran vimesheheni silaha za kujibu mapigo kwa tishio lolote lile
Aug 07, 2026 03:36Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa, kwa kutegemea utaalamu wa kiulinzi wa ndani ya nchi, Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vimesheheni kila vinachohitaji ili kutoa jibu kwa tishio lolote lile.
-
UNSC: Kundi la DAESH (ISIS) lingali ni tishio kubwa kwa usalama barani Afrika
Aug 07, 2026 03:35Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuwa, kundi la kigaidi la ISIS (DAESH) lingali ni tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa licha ya operesheni za kupambana na ugaidi zilizodhoofisha uongozi wake wa juu.
-
Tume ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi Nigeria yafunga akaunti za serikali ya jimbo
Aug 07, 2026 03:34Tume ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha nchini Nigeria, Economic and Financial Crimes Commission (EFCC), imeagiza kufungwa akaunti za Serikali ya Jimbo la Osun la Kusini Magharibi mwa nchi hiyo, ikieleza wasiwasi wake kuhusu fedha za umma zinazohusishwa na uchunguzi unaoendelea wa madai ya ubadhirifu wa fedha karibu Naira bilioni 11 ($8,080,000).
-
Taarifa ya nchi 8 za Kiarabu na Kiislamu yalaani jinai za Israel Ghaza
Aug 07, 2026 03:32Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi nane za Kiarabu na Kiislamu wametoa taarifa ya pamoja ambapo mbali na kulaani uchokozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liulazimishe utawala huo utekeleze majukumu yake na kuwawajibisha wale wanaokiuka haki za Wapalestina.
-
Pezeshkian: Iran inajulikana kama nchi yenye nguvu na inayoheshimika; maadui wanalenga nembo za nguvu zake
Aug 06, 2026 11:08Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa licha ya changamoto zinazoikabili nchi, Iran inatambulika kimataifa kama taifa lenye nguvu na linaloheshimika sana, huku akitahadharisha kuwa maadui wa taifa hili wanajaribu kudhoofisha alama za nguvu zake.
-
IRGC: Watu 8 wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi watiwa nguvuni kusini-mashariki mwa Iran
Aug 06, 2026 11:06Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza kuwa kimewatia nguvuni watu wanane wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran kufuatia oparesheni maalum mtawalia.