-
Ripoti: Mashambulio ya Marekani yaliua na kujeruhi mamia ya raia Yemen mwaka jana; Washington inaficha idadi kamili ya wahanga
Aug 06, 2026 11:04Mashambulio ya anga ya Marekani nchini Yemen yalisababisha vifo au majeraha kwa mamia ya raia mwaka jana, hata hivyo utawala wa Trump umeficha kwa makusudi idadi kamili ya waliofariki na kushindwa kuwasilisha kwa Bunge la nchi hiyo ripoti inayohitajika kuhusu wahanga wa mashambulio hayo.
-
Raia zaidi ya 300 waliotekwa nyara Nigeria waokolewa katika operesheni kubwa
Aug 06, 2026 11:02Nigeria imesema kuwa zaidi ya watu 300 waliotekwa nyara katika mashambulizi tofauti ya watu wenye silaha wameokolewa kupitia operesheni ya pamoja ya kiintelijensia na kiusalama.
-
Mbu vamizi azua hofu ya malaria kote barani Afrika
Aug 06, 2026 10:59Aina ya mbu vamizi inayoenea kwa kasi imezua hofu kote barani Afrika, huku wanasayansi wakionya kuwa inaweza kuchochea kuibuka upya kwa ugonjwa wa malaria katika miji mikubwa.
-
Malengo yanayofuatiliwa na Marekani katika kuzichochea nchi za Kiarabu zikabiliane na Iran
Aug 06, 2026 06:41Hata kama nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi hazitaki kuchochea mivutano katika eneo, kwa mujibu wa sera zao rasmi, lakini Marekani inajaribu kuzivuta katika makabiliano ya moja kwa moja na Iran.
-
Mgawanyiko kati ya Nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi Kuhusu Vita vya Marekani dhidi ya Iran
Aug 06, 2026 05:45Kwa mujibu wa gazeti la The Wall Street Journal, nchi za Kiarabu katika eneo la Ghuba ya Uajemi bado zimegawanyika pakubwa kuhusu namna ya kushughulikia vita vya kichokozi na kulazimishwa dhidi ya Iran.
-
Pezeshkian: Iran itaunga mkono maamuzi yatakayochukuliwa na viongozi wa Palestina
Aug 06, 2026 03:53Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaunga mkono mpango au uamuzi wowote utakaopitishwa na viongozi wa Palestina katika mchakato wa mazungumzo yanayoendelea, akithibitisha tena uungaji mkono thabiti wa Tehran kwa mapambano ya Palestina.
-
Trump anazidi kuchanganyikiwa kuhusu ulipizaji kisasi wa Iran, amkabili Hegseth kuhusu uhaba wa silaha
Aug 06, 2026 03:51Rais wa Marekani, Donald Trump, amezidi kukatishwa tamaa na kushindwa mara kwa mara kwa mashine ya kivita ya nchi hiyo kutokana na ulipizaji kisasi wa Iran na amemkabili Waziri wa Vita, Pete Hegseth, kuhusu uhaba wa silaha muhimu za Marekani.
-
Kituo kikubwa zaidi cha matibabu ya Ebola DRC huku maambukizi yakienea
Aug 06, 2026 03:49Kituo kikubwa zaidi cha matibabu ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kimefunguliwa wiki hii na wadau wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni hatua inayolenga kuimarisha mwitikio dhidi ya mlipuko wa sasa wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo unaoendelea kuenea kwa kasi katika jimbo la Ituri, mashariki mwa taifa hilo.
-
Interpol: Akili Mnemba (AI) inatumika katika 55% ya uhalifu wa mtandaoni barani Afrika
Aug 06, 2026 03:43Ripoti ya karibuni ya Polisi ya Kimataifa, Interpol, kuhusu tishio la uhalifu wa mtandaoni barani Afrika kwa mwaka 2026 imetoa onyo kali kuhusu jinsi teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inavyotumiwa kudhoofisha usalama wa kiuchumi na kijamii katika mataifa bara hilo.
-
Ruto asema serikali imetekeleza ahadi ilizowapa Waislamu wa Kenya
Aug 06, 2026 03:24Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali imetekeleza ahadi muhimu ilizotoa kwa jamii ya Waislamu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022.