-
Pezeshkian: Iran itaunga mkono maamuzi yatakayochukuliwa na viongozi wa Palestina
Aug 06, 2026 03:53Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaunga mkono mpango au uamuzi wowote utakaopitishwa na viongozi wa Palestina katika mchakato wa mazungumzo yanayoendelea, akithibitisha tena uungaji mkono thabiti wa Tehran kwa mapambano ya Palestina.
-
Trump anazidi kuchanganyikiwa kuhusu ulipizaji kisasi wa Iran, amkabili Hegseth kuhusu uhaba wa silaha
Aug 06, 2026 03:51Rais wa Marekani, Donald Trump, amezidi kukatishwa tamaa na kushindwa mara kwa mara kwa mashine ya kivita ya nchi hiyo kutokana na ulipizaji kisasi wa Iran na amemkabili Waziri wa Vita, Pete Hegseth, kuhusu uhaba wa silaha muhimu za Marekani.
-
Kituo kikubwa zaidi cha matibabu ya Ebola DRC huku maambukizi yakienea
Aug 06, 2026 03:49Kituo kikubwa zaidi cha matibabu ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kimefunguliwa wiki hii na wadau wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni hatua inayolenga kuimarisha mwitikio dhidi ya mlipuko wa sasa wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo unaoendelea kuenea kwa kasi katika jimbo la Ituri, mashariki mwa taifa hilo.
-
Interpol: Akili Mnemba (AI) inatumika katika 55% ya uhalifu wa mtandaoni barani Afrika
Aug 06, 2026 03:43Ripoti ya karibuni ya Polisi ya Kimataifa, Interpol, kuhusu tishio la uhalifu wa mtandaoni barani Afrika kwa mwaka 2026 imetoa onyo kali kuhusu jinsi teknolojia ya Akili Mnemba (AI) inavyotumiwa kudhoofisha usalama wa kiuchumi na kijamii katika mataifa bara hilo.
-
Ruto asema serikali imetekeleza ahadi ilizowapa Waislamu wa Kenya
Aug 06, 2026 03:24Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali imetekeleza ahadi muhimu ilizotoa kwa jamii ya Waislamu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022.
-
Waziri wa Afya wa Iran alaani shambulio la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo wa Lamerd Februari mwaka huu
Aug 05, 2026 12:18Waziri wa Afya wa Iran kwa mara nyingine tena amelaani shambulio lililofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo katika mji wa Lamerd mwanzoni mwa mashambulizi ya nchii hiyo na utawala katili wa Israel mwezi Februari mwaka huu hapa nchini lililosababisha vifo kuwajeruhi raia kadhaa.
-
Jeshi la Yemen lapiga meli nyingine ya mafuta ya Saudi Arabia katika Bahari Nyekundu
Aug 05, 2026 12:13Jeshi la Yemen limeishambulia meli ya mafuta ya Saudi Arabia katika sehemu ya kaskazini ya Bahari Nyekundu, baada ya meli hiyo kukiuka mzingiro wa baharini uliowekwa dhidi ya Saudi Arabia.
-
Ripoti: Marekani inazishinikiza nchi za Afrika kujiondoa ICC au kukabiliwa na madhara
Aug 05, 2026 12:11Utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani unazishinikiza nchi za Afrika kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na kutishia kuzichukulia hatua, huku Washington ikiongeza kasi ya kampeni yake dhidi ya mahakama hiyo.
-
Africa CDC yatoa tahadhari kufuatia mlipuko wa Ebola Kongo kushindwa kudhibitiwa
Aug 05, 2026 12:08Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika ( AFRICA CDC) kimetahadharisha kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unazidi kuwa nje ya udhibiti, huku vifo zaidi ya 1,700 vikirekodiwa ndani ya wiki 14 pekee. Hii ni katika hali ambayo juhudi za kuwafuatilia watu waliotangamana na wagonjwa zimeshindwa kudhibiti msambao wa virusi hivyo.
-
Hukumu ya kihistoria nchini Uingereza: Kupinga Uzayuni si chuki dhidi ya Wayahudi
Aug 05, 2026 12:03Katika uamuzi wa kihistoria uliotolewa jana Agosti 4, 2026, Mahakama Kuu ya Rufaa ya Ajira ya Uingereza ilikataa rufaa iliyowasilishwa na Chuo Kikuu cha Bristol dhidi ya msomi David Miller, ikithibitisha mfano wa kisheria unaotambua imani za kupinga Uzayuni kuwa ni itikadi ya kifalsafa inayolindwa chini ya Kifungu cha 10 cha Sheria ya Usawa ya Uingereza ya 2010.