-
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapasisha maazimio 5 ya kuunga mkono Palestina
Dec 06, 2025 04:24Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha kwa wingi maazimio matano kwa ajili ya Palestina, ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa shirika la UNRWA, kulaani vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuunga mkono haki za wakimbizi wa Kipalestina.
-
Wakimbizi wa Burundi watakiwa kuondoka Tanzania
Dec 06, 2025 04:20Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi kufuta hadhi ya ukimbizi na kuzifunga kambi za wakimbizi wa Burundi waishio mkoani kigoma kabla ya mwezi Juni mwaka ujao wa 2026.
-
Nchi za Kiislamu zaonya kuhusu mpango wa Israel wa kuwahamisha kwa nguvu raia wa Gaza
Dec 06, 2025 04:20Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi nane za Kiislamu wameeleza wasi wasi wao mkubwa kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya maafisa wa Israel kuhusiana na kufunguliwa kwa upande mmoja kivuko cha Rafah na kuwahamishia wakaazi wa Gaza nchini Misri.
-
Mapigano yaendelea mashariki mwa DRC licha ya Kagame na Tshisekedi kusaini makubaliano ya amani
Dec 06, 2025 04:19Mapigano makali yameendelea kushuhuudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku moja baada ya marais wa nchi hiyo kusaini makubaliano mapya ya amani mjini Washington Marekani.
-
Iran Yapangwa na Ubelgiji, Misri na New Zealand Kombe la Dunia la FIFA 2026
Dec 05, 2025 23:34Njia ya kuelekea Kombe la Dunia la FIFA 2026 sasa imewekwa wazi kwa Iran baada ya droo ya Ijumaa usiku mjini Washington, D.C. kuipanga Timu ya Taifa ya Soka ya Iran maarufu kama, Team Melli, katika Kundi G lenye mvuto na msisimko, pamoja na Ubelgiji, Misri na New Zealand.
-
Je, sera za chama tawala zimechangia kuenea chuki na ukatili dhidi ya Waislamu nchini India?
Dec 05, 2025 23:14Ghasia dhidi ya Waislamu nchini India zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni.
-
Uvamizi wa kijeshi wa Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi unaendelea
Dec 05, 2025 23:12Duru za habari zimeripoti kwamba wanajeshi na walowezi wa Kizayuni wameendelea kuvamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kuchoma moto nyumba za Wapalestina na kushambulia raia wasio na ulinzi.
-
Mwanamfalme wa Saudia: Tishio hasa la Asia Magharibi ni Israel, si Iran
Dec 05, 2025 23:12Turki Al-Faisal, mwanamfalme wa Saudi Arabia ambaye pia ni mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Saudia amesisitiza katika mkutano wa kimataifa huko Abu Dhabi kwamba, kinyume na wanavyodai baadhi ya watu, tishio hasa la eneo hili la Asia Magharibi si Iran bali ni utawala wa Kizayuni ambao ndio unaohatarisha utulivu wa eneo hili lote.
-
AfDB yatoa msamaha wa karibu dola milioni 18 za kwa Somalia
Dec 05, 2025 23:11Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema kuwa, imeidhinisha kusamehewa Somalia karibu dola milioni 18 na hivyo kufungua njia ya kufutwa kabisa mikopo yote ya nchi hiyo ambayo inajumuisha ya kipindi cha baina ya mwaka 2024 hadi 2039.
-
Mapigano ya silaha yafunga barabara kuu katika fukwe za magharibi mwa Libya
Dec 05, 2025 23:10Barabara kuu ya ufukweni inayopita katika mji wa Zawiya nchini Libya, yapata kilomita 60 magharibi mwa mji mkuu Tripoli, imefungwa kabisa tangu Alkhamisi jioni baada ya kuzuka mapigano na ufyatulianaji risasi kati ya makundi yenye silaha ya eneo hilo.