-
Muqawama wa Palestina watoa onyo baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya Israel tangu kusitisha mapigano
Aug 03, 2026 10:10Makundi ya Muqawama ya Palestina yametoa onyo kali baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya anga ya Israel tangu kusitisha mapigano Oktoba 2025, yakisema mashambulizi hayo yasiyokoma ni hujuma ya makusudi dhidi ya makubaliano ya kusitisha mapigano na ujumbe kwamba Israel haina nia ya kutimiza majukumu yake.
-
Kiongozi mkuu wa kidini wa Bahrain alaani mataifa ya Kiarabu kwa kutumikia ajenda za Marekani na Israel
Aug 03, 2026 10:08Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain, amezilaani nchi za Kiarabu na Kiislamu za kanda ya Magharibi mwa Asia kwa kuchangia katika njama za Marekani na Israel za kuimarisha migawanyiko katika eneo hilo.
-
Vibaraka wawili wa Mossad wanyongwa nchini Iran kwa kutoa taarifa za usalama kwa Israel
Aug 03, 2026 09:48Wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad, wamenyongwa kwa kosa la kutoa taarifa nyeti kuhusu jeshi na maeneo ya usalama ya Iran katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na Israel.
-
Malengo ya Julani katika kuanzisha uadui dhidi ya kundi la Hashd al-Shaabi la Iraq
Aug 03, 2026 08:39Abu Mohammad al-Julani, mtawala wa serikali ya mpito ya Syria, amedai katika matamshi tatanishi kuwa ana wasiwasi kuhusu uwepo wa makundi ya wanamgambo wa Iraq na vikosi vya Hashd al-Shaabi katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
-
Kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Haniya, Iran yasisitiza uungaji mkono wake kwa malengo ya Palestina
Aug 03, 2026 03:37Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa pili tangu alipouawa shahidi Ismail Haniya, ambapo mbali na kumuenzi mkuu huyo wa zamani wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS imesisitiza kuendelea kuunga mkono malengo matukufu ya Palestina na ulazima wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa ili kupunguza mateso ya watu wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi, sambamba na kufunguliwa kesi wahusika wa jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni
-
Sheikh Ibrahim Zakzaky apinga pendekezo la Trump kuhusu Gaza
Aug 03, 2026 02:46Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky, amelitaja pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu makubaliano ya usitishaji vita kati ya Israel na Hamas kuwa ni “uoga”, hasa kutokana na sharti linalodaiwa la kuitaka Hamas kusalimisha silaha zake.
-
Ripoti ya Middle East Monitor: Mwisho wa dhana ya Marekani ya 'kutoshindwa'
Aug 03, 2026 02:45Ripoti ya gazeti la Middle East Monitor imesema kuwa, Iran haiwezi kushindwa katika vita, na kwamba hali hiyo ni ukweli ambao Marekani na Israel haziwezi kuubadilisha hata kama watajitahidi kiasi gani.
-
New York Times: Umaskini wakithiri Marekani, pengo la kijamii lazidi kupanuka
Aug 03, 2026 02:43Gazeti la New York Times limeripoti kuongezeka umaskini nchini Marekani na kuongezeka pengo la kijamii miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo.
-
Maandamano makubwa ya kupinga sera zilizofeli za Benjamin Netanyahu
Aug 03, 2026 02:40Wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel wamefanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali wakipinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo wamezitaja kuwa zimeshindwa.
-
Baada ya Iran kuapa kuwa itajibu mapigo makali, Trump asitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu
Aug 02, 2026 13:15Rais wa Marekani Donald Trump amesema amefuta mashambulizi aliyotangaza kuwa yatafanywa dhidi ya Iran baada ya nchi za eneo kuomba yasitishwe wakati juhudi zinafanywa ili kufikia makubaliano, na kufuatia maonyo yaliyotolewa na Tehran kwamba uchokozi wowote mpya wa Marekani au Israel utakabiliwa na jibu la mapigo makali.