-
Katika mwezi wa Julai pekee Israel imeua Wapalestina zaidi ya 150 Ghaza
Aug 02, 2026 13:10Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza kuwa, katika mwezi Julai pekee, Wapalestina 152 waliuawa shahidi katika eneo hilo lililowekewa mzingiro, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo vya kila mwezi kuwahi kurekodiwa tangu ulipoanza mwaka huu.
-
Abdel Bari Atwan: Makamanda wa jeshi la Marekani wanahofia kurudiwa "tajiriba ya Vietnam"
Aug 02, 2026 13:06Abdel Bari Atwan, mchambuzi mashuhuri katika Ulimwengu wa Kiarabu ameashiria jinsi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyojiandaa kutoa kipigo kikali dhidi ya uchokozi wowote, na hofu ya makamanda wa kijeshi wa Marekani ya kujirudia tajriba ya Vita vya Vietnam, na kutaja sababu tano zilizomfanya Trump arudi nyuma katika kutekeleza vitisho vyake.
-
TPLF ya Tigray yaituhumu serikali ya Ethiopia 'kuanzisha vita vya wazi'
Aug 02, 2026 13:02Mamlaka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia zimeituhumu serikali ya shirikisho kuwa kuanzisha mashambulizi ya kijeshi siku ya Jumamosi, na kufufua hofu ya kurejea vitani.
-
Vita vya kinyama vya Israel Ghaza: Miili 40 ya watoto, 38 ya wanawake miongoni mwa iliyotolewa kwenye kifusi
Aug 02, 2026 12:57Shirika la Ulinzi wa Raia la Ghaza limesema, wafanyakazi wake walipata miili na mabaki ya watu 112 kutoka chini ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa na mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel katika kitongoji cha Sabra cha Jiji la Ghaza.
-
Changamoto mpya kwa Wasaudia kufuatia mzingiro wa majini wa Yemen
Aug 02, 2026 11:03Mzingiro wa majini wa Yemen dhidi ya Saudi Arabia, pamoja na kufungwa kwa Lango-Bahari la Bab al-Mandab kwa meli za mafuta za Saudia, vimetoa changamoto mpya kwa Wasaudia.
-
Mazuwari zaidi ya milioni nne wameingia Iraq tangu Muharram hadi sasa
Aug 02, 2026 03:27Mkuu wa Idara ya habari ya masuala ya usalama wa Iraq ametangaza kuwa wafanyaziara zaidi ya milioni nne wa kigeni wamewasili nchini humo tangu mwanzo wa mwezi wa Muharram, na kwamba zoezi la upokeaji mazuwari wanaokwenda kushiriki kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein AS lingali unaendelea.
-
Araqchi: Iran iko tayari kukabiliana na uvamizi wowote mpya wa Marekani
Aug 02, 2026 03:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ameonya dhidi ya kitendo chochote kipya cha uvamizi cha Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, akisisitiza kwamba Tehran iko tayari kikamilifu kukabiliana na makosa yoyote kama hayo.
-
Jenerali wa Marekani: Hatuna vikosi vya kutosha vya kuilinda Israel na makombora ya Iran
Aug 02, 2026 02:49Gazeti la The Washington Post limeandika: Jenerali mmoja mwandamizi wa Marekani barani Ulaya ameionya Pentagon kuwa Jeshi la Wanamaji halina vikosi vya kutosha vya kuweza kuendelea kuilinda Israel na makombora ya masafa marefu.
-
Kitengo cha "Kundi 26" cha RSF chajisalimisha kwa jeshi la Sudan
Aug 02, 2026 02:45Shirika la Habari la Sudan SUNA limetangaza kuwa, kitengo kimoja cha Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF kimejisalimisha kwa jeshi na kukabidhi wanajeshi wake na vifaa kamili vya kijeshi.
-
Shambulio la Israel dhidi ya maghala ya dawa Ghaza latajwa kuwa ni 'jinai ovu sana'
Aug 02, 2026 02:42Wizara ya Afya ya Ghaza imelaani kile ilichokiita "jinai ovu sana" iliyofanywa na vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel huko Deir el-Balah, ikisema shambulio hilo la Ijumaa asubuhi lililenga "maghala ya dawa" ya Hospitali ya Mashahidi wa Al-Aqsa, na kuyabomoa kikamilifu mawili kati ya maghala hayo.