-
Amnesty International: India inashiriki katika mauaji ya kimbari ya Gaza
Jul 31, 2026 03:20Katika ripoti mpya iliyotolewa jana, Julai 30, Amnesty International imefichua data za forodha kuhusu usafirishaji kutoka India kuelekea Israel, ikisema kwamba New Delhi imeendelea kusafirisha vipuri vya zana za kijeshi, risasi na vifaa kwa makampuni ya Israel licha ya hatari iliyo wazi ya silaha hizo kutumika katika mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.
-
Mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yaharibu ndege tatu za F-35 katika kambi ya Marekani huko Jordan
Jul 30, 2026 14:59Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetangaza kuwa limefanya mashambulizi ya makombora ya balestiki kwenye Kituo cha Anga cha Muwaffaq Salti kinachoendeshwa na jeshi la Marekani huko Azraq, nchini Jordan, na kuharibu ndege tatu za kivita za Marekani aina ya F-35 na kusababisha madhara makubwa kwa ndege nyingine tatu, katika operesheni ya kulipiza kisasi kwa shambulio la anga la Marekani lililoua watu watatu wa familia moja kwenye Kisiwa cha Qeshm nchini Iran.
-
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
Jul 30, 2026 14:53Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, amelazwa hospitalini na hana fahamu baada ya kuziraia akiwa mahakamani jana Jumatano. Hayo ni kwa mujibu wa mkewe na watu wengine wanaozihimiza mamlaka husika nchini Uganda kumwachilia huru baada ya kunyimwa dhamana mara kwa mara.
-
Shambulio la kinyama la US kisiwani Qeshm, Iran laua wazazi na mtoto wao mdogo
Jul 30, 2026 11:09Wanafamilia watatu, wakiwemo mama, baba na mtoto wao wa kiume wa miaka miwili, wameuawa shahidi katika shambulio la kinyama la anga la jeshi la kigaidi la Marekani lililolenga jengo la makazi kwenye Kisiwa cha Qeshm kusini mwa Iran.
-
Al-Nujaba ya Iraq yazionya US na Saudia: Shambulio lenu 'mtalilipia gharama kubwa'
Jul 30, 2026 11:05Harakat ya Hizbullah al-Nujaba ya Iraq imeonya kwamba maslahi ya Marekani na Saudi Arabia "yatalipa gharama kubwa" baada ya mashambulizi ya pamoja ya anga ya nchi hizo kulenga maeneo ya harakati hiyo ya Muqawama katika mikoa kadhaa ya Iraq usiku wa kuamkia jana, na kuua watu wasiopungua 20 na kujeruhi wengine wengi.
-
Upinzani DRC wakasirika baada ya Mahakama kumfungulia njia rais Tshisekedi kugombea muhula wa tatu
Jul 30, 2026 10:19Wanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, ambao ni wanachama wa muungano wa upinzani uliopewa jina la utani "C64", wamepinga vikali uamuzi wa Mahakama ya Katiba kuhusu sheria ya kura ya maoni, ambayo inaweza kumfungulia njia Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi kugombea urais kwa muhula wa tatu baada ya kura hiyo ya maoni.
-
Karibu nusu ya Wamarekani wanataka Netanyahu akamatwe licha ya propaganda za mamilioni ya dola
Jul 30, 2026 10:18Karibu nusu ya Wamarekani wanataka waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe licha ya propaganda zinazofanywa na utawala huo wa kizayuni ambazo zimeugharimu mamilioni ya dola.
-
WHO yaonya kuwa Uganda ingali iko katika hatari ya mripuko wa ebola
Jul 30, 2026 10:15Shirika la Afya Duniani, WHO leo limetoa indhari kwa Uganda kwamba ingali iko katika hatari kutokana na mripuko wa ugonjwa wa Ebola ulioenea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Kwa nini Marekani ilisimamisha vita dhidi ya Iran baada ya wiki mbili?
Jul 30, 2026 07:55Kufuatia wiki mbili za uhasama na baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuzungumzia uwezekano wa kupanua mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, mapigano kati ya pande hizi yalisimama ghafla.
-
Kwa nini Netanyahu atasajiliwa katika historia kama waziri mkuu mbaya zaidi wa utawala wa Kizayuni?
Jul 30, 2026 06:54Gazeti la Haaretz limeandika: Netanyahu atasajiliwa katika historia kama waziri mkuu mbaya zaidi wa utawala wa Kizayuni. Gazeti hilo limechapisha ripoti inayokosoa vikali utendaji wa Benjamin Netanyahu, likisisitiza kuwa atakumbukwa kama Waziri Mkuu mbaya zaidi wa utawala wa Kizayuni na kwamba madhara ya kiusalama na kiuchumi ya vita alivyovisababisha yataukabili utawala wa Israel kwa miaka mingi ijayo.