-
Al-Houthi: Umma wa Kiislamu unapaswa kujifunza kutokana na mapambano ya Iran dhidi ya Marekani na Israel
May 28, 2026 04:48Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa: Msimamo imara wa Iran unapaswa kuwa kichocheo cha kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
-
Ma'ariv: Maafisa 50 wa utawala unaotaka kujitenga Somaliland wamepewa nafunzo Israel
May 28, 2026 04:43Gazeti la Kiebrania la Ma'ariv limefichua kashfa mpya kuhusu uhusiano wa siri kati ya Tel Aviv na eneo linalotaka kujitenga huko kaskazini mwa Somalia, likiandika kwamba askari 50 wa "Somaliland" wamerejea Afrika baada ya kukamilisha kozi za mafunzo katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
HRW: Mamluki wa Colombia katika vita vya Sudan wanapewa mafunzo UAE
May 28, 2026 04:36Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kwamba wapiganaji mamluki kutoka Colombia wanapewa mafunzo katika kambi za kijeshi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kisha wanapelekwa Sudan ili kuwasaidia waasi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Ayatullah Khatami: Trump ana jeni ya kusema uongo
May 27, 2026 15:17Imamu wa Swala ya Idul Adh'ha iliyofanyika mapema leo mjini Tehran amesema: "Maadui wanatamani taifa la Iran lichoke, lakini kwa neema ya Mungu, wataingia kaburi na matarajio hayo."
-
Kwa nini Trump anataka Pakistan iwe na uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel?
May 27, 2026 13:29Chanzo kimoja cha habari cha Pakistan kimeripoti kuhusu upinzani wa wazi wa Islamabad dhidi ya ombi la Rais Donald Trump wa Marekani la kuitaka nchi hiyo ijiunge na mchakato wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, na kuongeza kuwa Islamabad inaiona hatua ya Washington kuwa jaribio la kutumia vibaya diplomasia ya "kusimamisha vita na Iran" ili kutoa mashinikizo katika kesi zisizohusiana.
-
Rais wa Iran ahimiza mshikamano wa Kiislamu dhidi ya Marekani na Israel katika mazungumzo na viongozi wa Kiislamu
May 27, 2026 10:57Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mheshimiwa Masoud Pezeshkian, ametoa wito wa kuimarishwa umoja na ushirikiano miongoni mwa nchi za Kiislamu, akisisitiza kuwa mshikamano wa Umma mzima wa Kiislamu ni nguzo muhimu katika kukabiliana na vitisho na changamoto zinazokabili eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Iran yasema ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita unathibitisha “nia ovu” ya Marekani,
May 27, 2026 10:53Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali ukiukwaji wa “wazi na usio na msingi” wa makubaliano ya kusitisha mapigano uliofanywa na Marekani katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Hizbullah yatekeleza operesheni 32 dhidi ya majeshi ghasibu ya Israel kusini mwa Lebanon
May 27, 2026 10:51Harakati ya Mapambano ya Kiislamu nchini Lebanon, Hizbullah, imetangaza kutekeleza mfululizo wa operesheni 32 za kijeshi dhidi ya majeshi vamizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yanayofanya chokochoko kusini mwa nchi hiyo.
-
Wapalestina wa Gaza katika jinamizi badala ya sherehe wakati wa Eid el-Adha
May 27, 2026 10:43Ikiwa leo ni sikukuu ya Eid El-Adha, Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel hawana cha kusherehekea bali wanakumbwa na jinamizi na masaibu yaliyosababishwa na utawala huo ghasibu.
-
Serikali ya DRC yasitisha safari za ndege Bunia kufuatia mlipuko wa Ebola
May 27, 2026 10:40Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imechukua hatua ya dharura kwa kusitisha safari zote za ndege zinazoingia na kutoka mjini Bunia, mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni juhudi za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa hatari wa Ebola.