-
Wanajeshi wa Madagascar waungana na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu
Oct 12, 2025 01:55Baadhi ya makundi ya wanajeshi wa Madagascar yamekaidi amri na kuungana na maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali, ambao wamekusanyika katika mji mkuu, Antananarivo, huku maandamano ya kupinga utawala wa Rais Andry Rajoelina yakizidi kupamba moto.
-
Mapigano makali yazuka kati ya majeshi ya Pakistan na Afghanistan kwenye mpaka wa nchi mbili
Oct 12, 2025 01:54Mapigano makali ya mpakani yamezuka kati ya majeshi ya Afghanistan na Pakistan huku vikosi vya nchi hizo mbili vikishambuliana kwa kutumia silaha nzito.
-
Amerika ya Kusini yagawanyika juu ya kiongozi wa upinzani Venezuela kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel
Oct 12, 2025 01:54Kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kiongozi wa upinzani nchini Venezuela María Corina Machado kumeibua hisia tofauti katika nchi za Amerika Kusini, huku baadhi ya viongozi wa nchi za eneo hilo wakipongeza hatua hiyo na wengine kulaani vikali kwa kuashiria matamshi na vitendo vya Machado vya kuchochea vurugu na machafuko au hata kuunga mkono kufanywa mashambulio na uvamizi wa kigeni dhidi ya nchi yake mwenyewe.
-
"Israel haiaminiki; Iran inaunga mkono kusimamishwa mauaji ya kimbari Gaza"
Oct 11, 2025 23:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inakaribisha kusitishwa kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza, huku akitoa indhari juu ya tabia ya kutokuwa na muamana Tel Aviv kwa kukiuka makubaliano kadhaa ya huko nyuma.
-
Uchaguzi wa Cameroon unafanyika leo huku Biya akitarajiwa kushinda muhula wa nane
Oct 11, 2025 22:53Wananchi wa Cameroon waliotimiza masharti ya kupiga kura leo Jumapili (12 Oktoba) wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kushiriki katika uchaguzi wa Rais.
-
Ripoti: Asilimia 90 ya miundombinu ya Gaza imeharibiwa
Oct 11, 2025 22:53Asilimia 90 ya miundombinu ya Gaza imeharibiwa kabisa baaada ya vita vya miaka miwili vilivyoanzishwa na utawala ghasibu wa Israel.
-
Umoja wa Mataifa: Watu milioni 25 wanakabiliwa na baa la njaa Sudan
Oct 11, 2025 22:52Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vimesababisha mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao na karibu milioni 25 kukumbwa na baa kubwa la njaa.
-
China: Marekani inakiuka mamlaka ya kujitawala ya mataifa mengine
Oct 11, 2025 22:51Fu cong, balozi na mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema kuhusiana na uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Venezuela kwamba, hatua hiyo ya Washington inakiuka vikali mamlaka ya kujitawala ya mataifa mengine.
-
Mgogoro katika Baraza la Mawaziri la Vita: Je, Ben-Gvir ataweza kusambaratisha baraza hilo la Netanyahu?
Oct 11, 2025 22:47Kufuatia kutangazwa makubaliano ya kusimamisha vita na kubadlishana mateka kati ya Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), Itamar Ben -Gvir Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni ametangaza kupinga vikali makubaliano hayo na kutishia kulimbaratisha baraza la mawaziri la Netanyahu.
-
Maelfu ya Wapalestina waendelea kurejea Gaza baada ya vita kusitishwa
Oct 11, 2025 09:19Maelfu ya raia wa Palestina waliokimbia makazi yao kufuatia mashambulio ya utawala wa kizayuni wa Israel wanaendelea kurejea kaskazini mwa mji wa Gaza kufuatia makubaliano ya usitishaji wa mapigano yaliyofikiwa wiki hii.