-
Uholanzi yatangaza kususia bidhaa zinazotoka Israel
Jul 22, 2026 09:47Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, serikali ya Uholanzi imeamua kupiga marufuku uingizaji, ununuzi na uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa katika maeneo ya vitongozi haramu vya walowezi wa utawala wa Kizayuni.
-
Zaidi ya watu 140 wafariki au kutoweka baada ya boti ya wakimbizi kukwama katika pwani ya Mauritania
Jul 22, 2026 09:45Zaidi ya watu 140 wamefariki dunia au kutoweka baada ya boti iliyokuwa imebeba wakimbizi kukwama karibu na mwambao wa Mauritania.
-
Seneta wa Marekani afichua uongo wa Trump kuhusu vita dhidi ya Iran
Jul 22, 2026 06:20Seneta Mark Warner wa Marekani amekiri kwamba "hakuna tishio lolote linalokaribia" kutoka kwa Iran dhidi ya Marekani.
-
Araqchi: Mwenendo wa wanadiplomasia wa Ufaransa Tehran haukubaliki
Jul 22, 2026 03:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amelaani mwenendo wa wanadiplomasia wawili wa Ufaransa mjini Tehran na kuutaja kuwa "usiokubalika," huku akiitaka Paris kuzuia kujirudia vitendo vinavyokwenda kinyume na taratibu za kidiplomasia.
-
Ripoti ya Umoja wa Mataifa yafichua: Afrika imeipiku Asia kama kitovu cha njaa duniani
Jul 22, 2026 03:20Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wenye makao yake makuu huko Roma ameonya kuwa, migogoro na machafuko katika masoko ya nishati duniani vinaweza kuwasukuma mamilioni zaidi ya watu kwenye njaa kwa kuzidisha gharama za mafuta, mbolea na chakula. Taarifa hii imetolewa huku ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ikionyesha kuwa maendeleo ya kimataifa dhidi ya njaa bado yako tete.
-
Ripoti ya UN: Njaa inapungua lakini bado iko juu ikilinganishwa na viwango vya kabla ya COVID
Jul 22, 2026 03:08Inakadiriwa kuwa watu milioni 645 walikumbwa na njaa mwaka jana duniani kote; idadi ambayo ni pungufu kwa watu milioni 14 ikilinganishwa na mwaka 2024, na wakati huo huo ni pungufu kwa watu milioni 43 ikilinganishwa na idadi ya watu walioathiriwa na njaa mwaka wa 2022. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani.
-
'Hatuogopi kuuawa shahidi': Mkuu mpya wa Hamas atoa ujumbe wa kwanza
Jul 22, 2026 03:05Khalil al-Hayya, mkuu mpya wa Idara ya Siasa ya Hamas, ametangaza katika ujumbe wake wa kwanza kama kiongozi wa harakati hiyo kwamba muqawama wa Palestina hautatishwa na mauaji ya wanawe au mauaji ya makamanda wake.
-
Misri yaishutumu Ethiopia kuwa inasimamia Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance kwa "njia ya kisiasa"
Jul 22, 2026 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty ameituhumu Ethiopia kuwa inasimamia Bwawa Kuu la Renaissance (GERD) kwenye Mto Nile "kwa njia ya kisiasa" kupitia hatua za upande mmoja dhidi ya Misri na Sudan.
-
Upinzani Cameroon wataka kuchukuliwe hatua ya kikatiba na kutangazwa nafasi wazi ya urais
Jul 22, 2026 03:01Kutokuwepo nchini kwa muda mrefu Rais wa Cameroon, Paul Biya, kunasababisha utata mkubwa nchini humo, zaidi ya siku 44 baada ya kuondoka nchini Juni 7, 2026, katika safari iliyoelezwa rasmi kama "kukaa kwa muda mfupi faraghani barani Ulaya," bila ya kurudi nyumbani hadi sasa.
-
Iran yaangamiza rada za jeshi la Marekani Magharibi mwa Asia, askari kadhaa wauawa
Jul 21, 2026 11:33Majeshi ya Iran yametekeleza operesheni za uharibifu mkubwa wa miundombinu kadhaa ya rada na mifumo ya mawasiliano ya kijeshi ya Marekani katika eneo hili sambamba na hujuma iliyofanya dhidi ya kambi tatu za Marekani nchini Kuwait, ikiwa ni hatua endelevu ya kulipiza kisasi dhidi ya ukiukaji unaofanywa na Marekani.