-
'Hatuogopi kuuawa shahidi': Mkuu mpya wa Hamas atoa ujumbe wa kwanza
Jul 22, 2026 03:05Khalil al-Hayya, mkuu mpya wa Idara ya Siasa ya Hamas, ametangaza katika ujumbe wake wa kwanza kama kiongozi wa harakati hiyo kwamba muqawama wa Palestina hautatishwa na mauaji ya wanawe au mauaji ya makamanda wake.
-
Misri yaishutumu Ethiopia kuwa inasimamia Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance kwa "njia ya kisiasa"
Jul 22, 2026 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty ameituhumu Ethiopia kuwa inasimamia Bwawa Kuu la Renaissance (GERD) kwenye Mto Nile "kwa njia ya kisiasa" kupitia hatua za upande mmoja dhidi ya Misri na Sudan.
-
Upinzani Cameroon wataka kuchukuliwe hatua ya kikatiba na kutangazwa nafasi wazi ya urais
Jul 22, 2026 03:01Kutokuwepo nchini kwa muda mrefu Rais wa Cameroon, Paul Biya, kunasababisha utata mkubwa nchini humo, zaidi ya siku 44 baada ya kuondoka nchini Juni 7, 2026, katika safari iliyoelezwa rasmi kama "kukaa kwa muda mfupi faraghani barani Ulaya," bila ya kurudi nyumbani hadi sasa.
-
Iran yaangamiza rada za jeshi la Marekani Magharibi mwa Asia, askari kadhaa wauawa
Jul 21, 2026 11:33Majeshi ya Iran yametekeleza operesheni za uharibifu mkubwa wa miundombinu kadhaa ya rada na mifumo ya mawasiliano ya kijeshi ya Marekani katika eneo hili sambamba na hujuma iliyofanya dhidi ya kambi tatu za Marekani nchini Kuwait, ikiwa ni hatua endelevu ya kulipiza kisasi dhidi ya ukiukaji unaofanywa na Marekani.
-
Iran yataka Baraza la Usalama la UN kulaani shambulizi la Marekani dhidi ya kituo cha nyuklia cha Darkhovin
Jul 21, 2026 11:31Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani bila kusita shambulizi la kombora lililofanywa na Marekani dhidi ya Kituo cha Nishati ya Nyuklia cha Darkhovin, na kuthibitisha tena kuwa shambulizi lolote au tishio dhidi ya vituo vya nyuklia vya amani ni kinyume na sheria za kimataifa.
-
Yemen yaonya Saudi Arabia kuhusu ‘matokeo mabaya’ iwapo uchokozi na kuzingirwa vitaendelea
Jul 21, 2026 11:28Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeonya utawala wa Saudi Arabia kuhusu “matokeo mabaya na makubwa” iwapo utaendelea kuongeza mashambulizi yake kwa kulenga miundombinu ya kiraia, na kuimarisha sera ya kuzingira bandari na viwanja vya ndege nchini Yemen.
-
Ukandamizaji wa sauti za kutetea Palestina nchini Ujerumani
Jul 21, 2026 11:25Mauaji ya halaiki yanayoendelezwa na utawala wa Israel huko Gaza kwa kiasi kikubwa yamefutwa kwenye vyombo vya habari vya Ujerumani na katika ajenda ya umma; hata hivyo, ukandamizaji wa sauti za kuunga mkono Palestina haujatoweka.
-
UN: Wakimbizi 144 wamefariki au kutoweka pwani ya Mauritania wakijaribu kufika Ulaya
Jul 21, 2026 11:21Wakala wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi (UNHCR) umetangaza kuwa watu 144 wameripotiwa kufariki dunia au kutoweka katika pwani ya Mauritania walipokuwa wakijaribu kuelwkea Ulaya.
-
Shambulio la Iran dhidi ya Kituo cha Marekani huko Al-Tanf, Syria: Hatua Isiyo na Mfano Wake na Yenye Jumbe za Pande Kadhaa
Jul 21, 2026 06:35Kwa mara ya kwanza tangu kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad miezi 19 iliyopita, vikosi vya jeshi la Iran vimeshambulia kwa njia ya anga eneo lililo ndani ya ardhi ya Syria.
-
Iran yathibitisha kupokea mapendekezo ya wapatanishi yanayolenga kupunguza mvutano
Jul 21, 2026 03:32Iran imethibitisha kupokea mapendekezo na maoni mbalimbali kutoka kwa wapatanishi kadhaa yanayolenga kupunguza mivutano na Marekani, huku Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baqaei, akisema kuwa Tehran inaendelea na juhudi za kidiplomasia sambamba na hatua zinazochukuliwa na vikosi vya ulinzi vya Iran.