-
Nigeria yataka haki baada ya raia wake wawili kuuawa katika machafuko Afrika Kusini
Jul 06, 2026 10:29Nigeria imetangaza kwamba raia wake wawili waliuawa mwezi uliopita nchini Afrika Kusini, kufuatia wimbi la maandamano ya chuki dhidi ya wahamiaji yaliyokuwa yakilenga wafanyakazi kutoka mataifa mengine ya Afrika nchini humo.
-
Idadi kubwa ya wapiga kura wa Marekani wasema vita vya Trump dhidi ya Iran havina tija
Jul 06, 2026 10:24Idadi kubwa ya wapiga kura nchini Marekani wanaamini kuwa vita vya Donald Trump dhidi ya Iran havijazalisha tija inayostahili gharama zilizotumika. Kulingana na utafiti mpya wa gazeti la Financial Times, hali hiyo inaashiria jinsi mzozo huo unavyozidi kudhoofisha uungaji mkono kwa mtawala huyo kuelekea uchaguzi wa katikati wa muhula mwezi Novemba.
-
Ubelgiji yalaani FIFA kuhusu kuruhusiwa kwa mshambuliaji wa Marekani licha ya kadi nyekundu
Jul 06, 2026 07:32Shirikisho la Soka la Ubelgiji limeonyesha ghadhabu kubwa kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, kumruhusu mshambuliaji wa Marekani, Folarin Balogun, kushiriki katika mechi muhimu ya hatua ya 16 bora dhidi ya Ubelgiji siku ya Jumatatu, licha ya mchezaji huyo kuonyeshwa kadi nyekundu katika mzunguko uliopita.
-
Mamilioni wafurika Tehran kwa mazishi ya kihistoria ya Kiongozi Muadhamu aliyeuawa Shahidi
Jul 06, 2026 05:59Umati wa waombolezaji umefurika barabarani katika mji mkuu wa Iran huku msafara wa mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, yakianza. Tukio hili linaelezwa na maafisa kama mkusanyiko mkubwa zaidi wa umma kuwahi kushuhudiwa katika historia.
-
Mkuu wa Jeshi: Iran haitachoka kuwafuatilia waliomuua Kiongozi wetu
Jul 06, 2026 03:50Iran haitawahi kuacha azma yake ya kutafuta haki na kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu), zaidi ya miezi minne tangu alipouawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na Israel.
-
Jihad Islami: Nguvu ya Muqawama inatokana na kujitolea Kiongozi Shahidi
Jul 06, 2026 03:42Msemaji wa harakati ya Muqawama ya Jihad Islami ya Palestina amesisitiza kuhusu “matamanio matukufu” ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, akisema kuwa nguvu ya Mhimili wa Muqawama inatokana na kujitolea kwake maishani.
-
El Niño kuibua hatari ya maafa barani Afrika
Jul 06, 2026 03:29Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa (WMO) limetangaza kuwa hali ya mkondo joto baharini au El Nino imeanza katika ukanda wa kitropiki wa bahari ya Pasifiki na inatarajiwa kuimarika kwa kasi kati ya mwezi huu wa Julai na Septemba 2026.
-
Kesi za Ebola DRC zapanda na kuvuka 1,500, vifo vyafikia 473
Jul 06, 2026 03:20Idadi ya kesi zilizothibitishwa za ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imevuka 1,500 siku ya Ijumaa, baada ya maambukizi mapya zaidi ya 40 kuripotiwa, kulingana na takwimu rasmi, huku juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo na ufuatiliaji zikiendelea.
-
IOM : Mashambulizi ya RSF yanaweza kuifanya El Obeid nchini Sudan kuwa 'El Fasher nyingine'
Jul 06, 2026 02:48Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetahdharisha kuwa mji wa El-Obeid nchini Sudan, ambao ni makao makuu ya Jimbo la Kordofan Kaskazini, unaweza kukumbwa na hatima sawa na ile iliyoupata mji wa El Fasher katika jimbo jirani la Darfur Kaskazini iwapo mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa kikosi cha Msaada wa Haraka, Rapid Support Forces (RSF) yataendelea.
-
Pezeshkian: Kufa shahidi Ayatullah Khamenei kumetoa msukumo kwa Waislamu kudumisha umoja
Jul 05, 2026 11:15Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hayati Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuuawa kwake shahidi, vimewapa Waislamu kote duniani hamasa katika harakati zao za kudumisha umoja na mshikamano.