-
Mkuu wa Jeshi: Iran haitachoka kuwafuatilia waliomuua Kiongozi wetu
Jul 06, 2026 03:50Iran haitawahi kuacha azma yake ya kutafuta haki na kulipiza kisasi dhidi ya wauaji wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu), zaidi ya miezi minne tangu alipouawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na Israel.
-
Jihad Islami: Nguvu ya Muqawama inatokana na kujitolea Kiongozi Shahidi
Jul 06, 2026 03:42Msemaji wa harakati ya Muqawama ya Jihad Islami ya Palestina amesisitiza kuhusu “matamanio matukufu” ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, akisema kuwa nguvu ya Mhimili wa Muqawama inatokana na kujitolea kwake maishani.
-
El Niño kuibua hatari ya maafa barani Afrika
Jul 06, 2026 03:29Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa (WMO) limetangaza kuwa hali ya mkondo joto baharini au El Nino imeanza katika ukanda wa kitropiki wa bahari ya Pasifiki na inatarajiwa kuimarika kwa kasi kati ya mwezi huu wa Julai na Septemba 2026.
-
Kesi za Ebola DRC zapanda na kuvuka 1,500, vifo vyafikia 473
Jul 06, 2026 03:20Idadi ya kesi zilizothibitishwa za ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imevuka 1,500 siku ya Ijumaa, baada ya maambukizi mapya zaidi ya 40 kuripotiwa, kulingana na takwimu rasmi, huku juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo na ufuatiliaji zikiendelea.
-
IOM : Mashambulizi ya RSF yanaweza kuifanya El Obeid nchini Sudan kuwa 'El Fasher nyingine'
Jul 06, 2026 02:48Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetahdharisha kuwa mji wa El-Obeid nchini Sudan, ambao ni makao makuu ya Jimbo la Kordofan Kaskazini, unaweza kukumbwa na hatima sawa na ile iliyoupata mji wa El Fasher katika jimbo jirani la Darfur Kaskazini iwapo mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa kikosi cha Msaada wa Haraka, Rapid Support Forces (RSF) yataendelea.
-
Pezeshkian: Kufa shahidi Ayatullah Khamenei kumetoa msukumo kwa Waislamu kudumisha umoja
Jul 05, 2026 11:15Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hayati Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuuawa kwake shahidi, vimewapa Waislamu kote duniani hamasa katika harakati zao za kudumisha umoja na mshikamano.
-
Maafisa wa muqawama wafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pambizoni mwa mazishi ya Kiongozi Shahidi Khamenei
Jul 05, 2026 11:10Maafisa kutoka harakati ya muqawama wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, na kuwasilisha salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika mashambulizi ya kigaidi a Marekani na Israel dhidi ya Iran Februari 28 mwaka huu.
-
Harakati ya Ansarullah yalaani vitisho vya muungano wa Saudi Arabia; yasema ni ishara ya kushindwa Riyadh
Jul 05, 2026 11:04Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vitisho vya hivi karibuni vya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, akisema kuwa vinafichua kufeli Riyadh kisiasa na kijeshi pamoja na kushindwa kwake kusambaratisha mapambano ya Yemen licha ya nchi hiyo kuathirikwa kwa miaka mingi na vita na mzingiro.
-
Dakta Abu Safiya anakabiliwa na hali mbaya katika gereza la Israel
Jul 05, 2026 11:00Shirika la Kimataifa la Haki za binadamu limearifu kuwa Dakta Hussam Abu Safiya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza ambaye amekuwa mikononi mwa Israel tangu mwaka 2024 anakabiliwa na tishio kubwa kwa maisha yake.
-
Korea Kaskazini yalifanyia majaribio kombora la kimkakati la kruzi na silaha nyingine
Jul 05, 2026 10:57Korea Kaskazini imelifanyia jaribio kombora la kimkakati la kruzi na silaha nyingine kutoka katika meli yake mpya ya kivita ya Kang Kon yenye yenye uzito wa tani 5,000 na refu wa mita 140. Shirika Kuu la Habari la Korea Kaskazini KCNA leo limetangaza kuwa Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alisimamia majaribio hayo siku ya Ijumaa.