-
Baghaei: Iran inafuatilia hatua kwa hatua utekelezaji wa Marekani wa MoU
Jul 01, 2026 03:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Tehran itafuatilia, dakika kwa dakika, iwapo Marekani itazingatia makubaliano ya maelewano (MoU) ya kumaliza vita, na akaonya kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitatekeleza wajibu wake chini ya makubaliano hayo ikiwa ni upande mmoja pekee unaoyatekeleza.
-
Wabunge wa Israel warushiana makonde ndani ya ukumbi wa Bunge
Jul 01, 2026 03:35Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kutokea vurugu na mapigano ndani ya Bunge la utawala huo (Knesset), kufuatia kufutwa sheria iliyokuwa inahusu wafungwa wa Kipalestina.
-
Waziri: Iran itajibu ukiukaji wowote wa usitishaji vita
Jul 01, 2026 03:31Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakiuna shaka yoyote kwamba, Tehran itajibu kwa nguvu zote ukiukaji wowote ule wa usitishaji vita.
-
Umoja wa Mataifa: Unyanyasaji wa kingono na mauaji yaongezeka DRC
Jul 01, 2026 03:28Uchunguzi katika mikoa miwili ya mashariki mwa DRC ya Kivu Kaskazini na Kusini waonesha ukikwaji wa haki za binadamu umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
-
Rais Pezeshkian asema Iran itatekeleza mapatano ikiwa Marekani itafanya hivyo
Jun 30, 2026 11:31Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa makubaliano yoyote kati ya Iran na Marekani lazima yajikite katika heshima ya pande zote na ahadi za pamoja, na si kwa kutumia vitisho au shinikizo la upande mmoja.
-
Oman yaunga mkono mpango wa Iran wa kutoza ‘ada za huduma’ katika Lango la Hormuz
Jun 30, 2026 11:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr al-Busaidi, ametangaza msimamo wa nchi yake kuunga mkono mpango wa Iran wa kuanzisha utaratibu wa “ada za huduma za baharini” kwa meli zinazopita katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Jeshi: Mazishi ya Kiongozi Shahidi yatakuwa mwamko wa kimataifa dhidi ya ugaidi na jinai za Marekani na Uzayuni
Jun 30, 2026 11:23Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesema kuwa sherehe za kitaifa za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zitatumika kama jukwaa la harakati za kimataifa za kulaani ugaidi na maandamano hai dhidi ya jinai zinazofanywa na mhimili wa Marekani na Uzayuni.
-
Mjumbe wa Palestina ataka jumuiya ya kimataifa izuie hatua za Israel za kupora ardhi ya Palestina
Jun 30, 2026 11:21Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa kuacha kauli za kulaani pekee na badala yake kuchukua hatua za kivitendo ili kusitisha mpango wa Israel wa kupora ardhi za Palestina.
-
Polisi wa Afrika Kusini wakabiliana na waandamanaji wanaopinga wageni
Jun 30, 2026 11:18Mamlaka nchini Afrika Kusini zimeimarisha ulinzi kwa kupeleka vikosi vya polisi katika miji mikuu ya nchi hiyo, kufuatia wimbi la maandamano dhidi ya raia wa kigeni wasio na nyaraka rasmi za ukaazi.
-
Kwa nini makubaliano ya Washington yamefungua njia ya fitina mpya nchini Lebanon?
Jun 30, 2026 05:53Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon ametahadharisha kuhusu njama mpya dhidi ya Lebanon akiashiria makubaliano ya Washington kati ya serikali ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwahutubu wananchi wa nchi hiyo kwa kusema: "Enyi watu wa Lebanon, hii ni njama hatari."