Oct 03, 2023 02:45 UTC
  • Mkutano wa Kimataifa wataka hatua zichukuliwe kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

Mkutano wa kimataifa kuhusu chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) umefanyika nchini Qatar huku mmoja wa waandalizi wake akitoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja za kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na athari zake "haribifu".

Mkutano huo uliopewa anwani ya "Historia ya Ulimwengu na Mienendo ya Chuki dhidi ya Uislamu", umefanyika katika Chuo Kikuu cha Georgetown tawi la Qatar

Katika hotuba ya kuhitimisha mkutano huo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Georgetown Qatar, Safwan M. Masri ameashiria haja ya kufanyiikka juhudi za pamoja kwa ajili ya kukomesha chuki dhidi ya Uislamu.

Amesema kuwa tukio hilo limetoa "mchango katika juhudi za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu, kupinga athari zake haribifu, na kuchukua hatua athirifu zinazojumuisha wanaharakati, waelimishaji na wasanii ili kukabiliana na tatizo hilo.

Washiriki katika mkutano huo wa siku mbili walijishughulisha na mazungumzo, kuuliza maswali, na kuchunguza mizizi ya kiitikadi ya mielekeo mingi ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Kongamano hilo liliwakutanisha pamoja wasomi wenye ushawishi mkubwa, watendaji, na waandishi wa habari, kati yao wanafunzi wa zamani wa Georgetown na wanafunzi wa Qatar wa Chuo Kikuu cha Georgetown ambao wamechangia ufahamu wao.

"Mkutano huo uliishia katika mjadala wa ngazi ya juu wa meza ya pande zote ambapo washiriki wamechunguza masuluhisho yanayowezekana ili kupambana na chuki dhidi ya Uislamu."

Washiriki walisema, licha ya Uislamu kuwa neno la kawaida katika muongo mmoja uliopita, ni wajibu kwa wasomi na watendaji kuchunguza historia ya chuki dhidi ya Uislamu ili kuelewa tatizo hilo kikamilifu.

Tags