Dec 03, 2023 08:00 UTC
  • HAMAS yaendelea kuitwanga kwa makombora Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni + Video

Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu HAMAS zimetangaza usiku wa kuamkia leo kwamba umeendelea kuipiga kwa makombora miji ya utawala wa Kizayuni ukiwemo mji mkuu Tel Aviv ili kujibu jinai za israel dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kutokea mashambulio hayo na kusema kwamba zaidi ya miripuko mikubwa 20 imesikika Tel Aviv.

Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza pia kuwa, moja ya makombora ya HAMAS limepiga kwenye kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Modi'in cha magharibi mwa Ramallah na shambulio hilo ni kali kiasi kwamba utawala wa Kizayuni umelazimika kupeleka huko idadi kubwa ya askari wake.

Vyombo hivyo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza pia kuwa, makombora mengine mawili yamepiga kwenye barabara kuu ya 443 inayounganisha miji ya Tel Aviv na Baytul Muqaddas. 

Vyombo hivyo vya habari za Kizayuni aidha vimetangaza kuwa, katika wimbi jipya la mashambulizi yake ya makombora, HAMAS imeupiga kwa makombora mengi sana mji ya Tel Aviv na maeneo yanaouzunguka mji huo.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya Israel, kwa uchache makombora 100 ya HAMAS yamevurushiwa upande wa mji wa Tel Aviv na vitongoji vyake kutokea Ghaza, ikiwa ni katika wimbi hili jipya la mashambulio ya wanamapambano wa Palestina ya kujibu jinai za Wazayuni. 

Brigedi za al Qassam zimesambaza video zinazoonesha sehemu ya mashambulio yake hayo ya makombora dhidi ya maeneo ya Wazayuni ukiwemo mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, Tel Aviv. Moja ya mikanda ya video uliorekodiwa mjini Tel Aviv unaonesha kombora moja likipiga eneo la Gush Dan mjini humo.

Sambamba na hayo HAMAS imesema wazi kwamba hakuna mabadilishano yoyote ya mateka yatakayofanyika ila baada ya utawala wa Kizayuni kukomesha kikamilifu jinai zake dhidi ya wananchi wa Ghaza.