Apr 23, 2024 08:32 UTC
  •  UN yatoa  onyo kali kuhusu madhara ya vita kwa afya na akili za watu wa Gaza

Umoja wa Mataifa (UN) umetahadharisha na kutoa onyo kali kabisa kuhusu madhara ya vita kwa afya na akili ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Kwa mujibu wa kanali ya habari ya televisheni ya Al Jazeera, Tlaleng Mofokeng, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa, akizungumzia mauaji ya kimbari ya muda mrefu yanayofanywa na utawala haramu wa Kizayuni na uharibifu wa miundombinu ya afya na matibabu ya Ukanda wa Gaza wakati wa siku 200 za mashambulizi ya mabomu, alisema kwamba shinikizo kubwa la kisaikolojia lilisababisha wasiwasi na magonjwa mengine ya akili yatabadilika na ni muhimu sana kufikiri juu ya hili suala kwani ni muhimu kwa watu wa ukanda wa Gaza Mofokeng aliongeza kwa kusema kwamba:  kuwa mfumo wa huduma za afya huko ukanda wa  Gaza umeharibiwa kabisa na afya imedhoofisha afya za watu hao huko Gaza.  

Msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) pia ameitaja hali ya watoto katika Ukanda wa Gaza kuwa ni chungu na ya kusikitisha na kuonya kuhusu matokeo ya muda mrefu ya uchokozi wa utawala  haramu wa Kizayuni katika afya ya kimwili, maendeleo na afya ya akili ya watoto katika mkoa huu.

Tennes Ingram, Msemaji wa mkuu wa (UNICEF)  huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza ameongeza kuwa: watoto wa Ukanda wa Gaza wametangatanga bila ya kuwa na sehemu salama ambapo wanaweza kujikinga na migogoro na majeraha yanayoendelea kutokana na vita vya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa eneo hilo uko Gaza.

Wakati huo huo, msemaji huyo wa mkuu wa (UNICEF) amedokeza kuwa kutokana na ari kubwa iliyopo miongoni mwa wakaazi wa ukanda wa Gaza, licha ya hali ngumu wanayokabiliana nayo watu wa Gaza wa eneo hilo, anaona kupata matumaini kwa watu hao.

Jinai za utawala haramu ghasibu wa Israel katika ukanda wa Gaza zinatekelezwa kwa mwanga wa kijani wa Marekani, huku Ikulu ya Marekani ikipuuza jinai hizo dhidi ya binadamu za utawala haramu wa Kizayuni, hivi karibuni imekubali kutuma dola bilioni 26 za  kijeshi za msaada kwa utawala huu haramu wa kizayuni.