Mar 05, 2020 03:42 UTC
  • Haniya: Shahidi Soleimani alikuwa na nafasi ya

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) aliyeuliwa shahidi alikuwa na nafasi muhimu na ya msingi katika kuunga mkono muqawama.

Ismail Haniya ameyasema hayo akiwa mjini Moscow, Russia na akabainisha kwamba: Iran ni nchi iliyo mhimili mkuu katika kuunga mkono muqawama wa Palestina katika kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel, na Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuliwa shahidi alikuwa na nafasi kuu katika kuunga mkono suala la Palestina.

Ismail Haniya akihutubia katika mazishi ya shahidi Qassem Soleimani mjini Tehran

Haniya ameongeza kuwa: Marekani na Wazayuni wanadhani kwamba, kwa kuwaua kigaidi shakhsia muhimu wataweza kuuzuia muqawama katika eneo, lakini ni kinyume chake, kwa sababu kila mauaji yanayofanywa yanazidisha uimara na uthabiti wa muqawama, na viongozi wapya wanaokuja wanaendeleza njia ya wale waliouawa.

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas aidha amesema, hali katika Ukanda wa Gaza ni ya janga na maafa na akaongeza kuwa, Hamas imewasilisha mapendekezo kadhaa kwa Russia kuhusu namna ya kulisaidia eneo hilo katika nyuga mbali mbali.../

Tags