Dec 28, 2020 12:20 UTC
  • Hizbullah: Luteni Jenerali Qassim Suleimani ni shahidi wa Ulimwengu wa Kiislamu

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Luteni Jenerali Qassim Suleimani ni shahidi wa Ulimwengu wa Kiislamu na mashahidi wa mhimili wa muqawama.

Samahat Sheikh Naim Qassim amesema hayo katika makala  iliyochapishwa na Mtandao wa Habari wa al-Ah'd ambapo amemtaja shahidi Qassim Suleimani kuwa kamanda aliyefaulu katika medani ya jihadi na vita ambaye alikuwa akiandaa mipango kwa umakini mkubwa na ambaye alipata mafanikio makubwa katika operesheni dhidi ya maadui.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesem kuwa, shahidi Qassim Suleimani alikuwa pia mwanasiasa mjuzi na mwenye utambuzi kuhusiana na mahesabu ya kieneo na kimataifa.

Samahat Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon

 

Aidha Shekh Naim Qassim amesema kuwa, shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani alikuwa mtu mwenye kupima mambo kwa umakini mkubwa na ambaye alikuwa pia na muono wa mbali katika masuala ya kisiasa na kijeshi.

Luteni Jenerali Qassem Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Suleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Tags