May 01, 2023 06:55 UTC
  • Kiongozi wa Daesh auawa katika operesheni ya jeshi la Uturuki nchini Syria

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alitangaza jana Jumapili jioni kwambau kiongozi wa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh), ameuawa katika operesheni ya kijasusi ya Uturuki nchini Syria.

Erdogan amesema - katika mahojiano ya moja kwa moja na ya televisheni- kwamba "shirika la ujasusi wa Uturuki limekuwa likimfuatilia kwa muda mrefu anayejulikana kama Abu al-Hussein al-Qurashi, kiongozi wa ISIS (Daesh), na lilimuawa jana katika operesheni nchini Syria."

Mwezi Novemba mwaka jana kundi la kigaidi la Daesh lilitangaza katika mkanda wa sauti kwamba limemteua Abu al-Hussein al-Husseini al-Qurashi kama eti "khalifa wa Waislamu", na kuwa kiongozi wa nne wa kundi hilo.

Tangazo hilo lililitolewa baada ya kundi hilo kuthibitisha kuuawa kwa kiongozi wake wa tatu, Abu al-Hasan al-Hashemi al-Qurashi, katika operesheni iliyofanywa nchini Syria.

Kundi la kigaidi la ISIS, ambalo lilidhibiti maeneo makubwa ya Syria na Iraqi mnamo 2014, lilipigwa na kushindwa kwa mara ya kwanza nchini Iraqi mnamo 2017 na kisha huko Syria mnamo 2019, na kupoteza maeneo yake yote kuu ya udhibiti. 

Kundi hilo lilikuwa likifadhiliwa na Marekani na washirika wake wa kikanda na Kimagharibi kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya Syria. 

Tags