May 01, 2023 07:23 UTC
  • Wanajeshi wa Israel washambulia Hospitali Bait Laham na Msikiti wa Al-Aqsa

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameshambulia hospitali moja mjini Bait Laham mapema leo Jumatatu na kurusha mabomu ya kutoa machozi ndani ya hospitali hiyo.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, wanajeshi vamizi wa Israel mapema leo ​​wameishambulia Hospitali ya Jimbo la Beit Jala katika mkoa wa Bait Laham na kurusha mabomu ya kutoa machozi ndani ya kituo hicho cha afya, suala lililosababisha usumbufu mkubwa wa kupumua kwa idadi kubwa ya wagonjwa.

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Palestina imelaani vikali shambulio na jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni huko Bait Laham.

Wakati huo huo, walowezi wa Kizayuni wameushambulia tena Msikiti wa al-Aqsa asubuhi ya leo chini ya himaya ya askari usalama wa Israel.

Msikiti wa Al-Aqsa umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na Wazayuni katika wiki kadhaa za hivi karibuni hususan katika mwezi mtukufu uliomalizika wa Ramadhani. Wazayuni hao wanataka kuugawawa kieneo na kiwakati msikiti huo na kuwaruhusu Wazayuni kulinajisi eneo hilo tukufu la Waisalmu. 

Tags