May 18, 2023 01:08 UTC
  • Mawaziri wa utawala wa Kizayuni watoa wito wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa baadhi ya mawaziri na wajumbe wa bunge la utawala haramu wa Israel, Knesset, wametoa wito wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya maandamano ya bendera.

Maandamanio ya bendera hufanyika kila mwaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu sehemu ya zamani ya Quds Tukufu na utawala wa Kizayuni katika vita vya mwaka 1967. Wazayuni wanadai kuwa, Quds Tukufu (Jerusalem) ndio mji mkuu wa utawala huo, lakini wananchi wa Palestina wanasisitiza kuwa Quds itakuwa mji mkuu wa nchi yao.

Shirika la habari la Mehr limevinukuu vyombo vya habari vya Palestina kwamba, mawaziri na wajumbe wa Knesset (Bunge la utawala wa Kizayuni) wamewasilisha ombi rasmi, wakitaka kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqwa leo Alkhamisi wakati wa maandamano ya bendera.

Wakati huo huo, gazeti la lugha ya Kiebrania Yedioth Ahronoth pia limesisitiza kwamba Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel alitarajiwa kuitisha mkutano wa kutathmini hali ya mambo kabla ya maandamano ya leo ya bendera, ambayo yeye mwenyewe ameamua kushiriki.

Inasemekana kuwa "Bezalel Smotrich", Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ambaye pia anahesabiwa kuwa mmoja wa Wazayuni wenye misimamo mikali, atashiriki katika hujuma dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa hii leo Alkhamisi.

Wakati huo huo, idara ya vyombo vya habari ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya Hamas, imesambaza video mpya katika mkesha wa kinachoitwa "maandamano ya bendera", na kuwaonya Wazayuni kwamba "Upanga wa Quds kamwe haujarudishwa kwenye kifuniko chake", jambo ambalo ni ukumbusho wa mashambulizi ya makombora ya wapigania ukombozi wa Palestinai dhidi ya mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds (Jerusalem) wakati wa maandamano ya bendera mwaka 2021.

Tags