Jun 11, 2023 07:57 UTC
  • Chama cha Jordan: Njama mpya za Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa ni kutangaza vipya

Chama cha Islamic Action Front cha Jordan kimetangaza kuwa, njama mpya za utawala wa muda wa Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na hujuma zake dhidi ya eneo hilo takatifu ni kutangaza vita.

Chama hicho kimelaani vikali hatua za kila uchao cha utawala ghasibu wa Israel dhidi ya msikiti wa al-Aqswa na kuueleza kwamba, kunapaswa kuchukuliwa hatua za kukabiliana na mipango yay Israel dhidi ya eneo hilo takatifu.

Omit Helivi", mwakilishi wa chama cha Likud katika Bunge la Israel (Knesset), hivi karibuni aliwasilisha mpango ambao msingi wake ni kuugawanywa msikiti huo kimuda na kimahaali.

Wazayuni wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaounga mkono njama za kuubomoa msikiti mtukufu wa Al-Asqa na kujenga mahali pake hekalu bandia la Kiyahudi wamependekeza mpango hatari na wa ubaguzi wa kimbari kwa madhumuni ya kupagawanya mahali hapo patakatifu.

Katika mpango huo wa kibaguzi wa makundi na jumuiya za Kizayuni wa kuugawanya msikiti wa Al-Aqsa baina ya Waislamu na Mayahudi imesisitizwa kuwa, kutokana na mgawanyo huo ni sehemu ya zamani tu ya uwanja wa kusalia ndiyo itakayobaki kuwa ya Waislamu.

Walowezi wa Kizayuni

 

Awamu mpya ya harakati na chokochoko zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa lengo la kuyadhibiti hatua kwa hatua maeneo ya Palestina hususan ya Kiislamu ukiwemo msikiti wa Al-Aqsa, imechukua mkondo na muelekeo hatari zaidi.

Katika miaka ya karibuni kuugawanya msikiti wa Al-Aqswa kimatumizi kwa sura ya mahali na wakati ndio ajenda kuu ambayo viongozi wa Israel wamekuwa wakiifanyia kazi; na hivi sasa uporaji wa haki za wananchi wa Palestina unaofanywa na utawala huo ghasibu umeshadidi na kupamba moto zaidi kutokana na Wazayuni kuutumia muda wao mwingi kwenye kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Tags