Wanamgambo wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Boko haram wamewateka nyara watu 11 katika eneo moja la kaskazini mwa Cameroon.
Viongozi wa serikali ya Niger wametoa indhari kwa raia wa nchi hiyo kujihadhari na uharamia unaofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram wa kuteka watu nyara na kudai kikomboleo cha fedha.
Idadi ya watu waliuawa kaskazini mwa Nigeria baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram kuwashambulia watu waliokuwa wakitoka msibani imeongezeka na kufikia 65.
Watu wasiopungua 23 wameuawa kaskazini mwa Nigeria na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram kufanya mashambulio katika maeneo hayo.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria ametangaza kuwa, kwa uchache watoto 8,000 wanatumiwa na kundi la kigaidi la Boko Haram kama askari vitani.
Kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram limeua askari 11 wa Chad, katika eneo la Ziwa Chad.
Wanajeshi 15 wa Nigeria wameuawa katika shambulizi linaloaminika kutekelezwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi.
Watu wasipungua 30 wameuawa katika mashambulizi kaskazini mwa Nigeria katika hujuma inayoaminika kutekelezwa na magaidi wakufurishaji wa Boko Haram.
Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) katika eneo la Magharibi mwa Afrika (ISWA) limedai kwamba limeua makumi ya askari wa Nigeria huko kaskazini mwa nchi hiyo.
Wanajeshi wasiopungua 17 na raia tisa wameuawa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram huko Darak kaskazini mwa Cameroon.