-
Burkina Faso yarefusha muda wa utawala wa kijeshi kwa miaka mitano baada ya mashauriano ya kitaifa
May 26, 2024 07:07Kanali Moussa Diallo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mchakato wa mazungumzo ya kitaifa ya Burkina Faso amesema kuwa wameainisha muda wa kipindi cha mpito kuwa miezi 60 kuanzia Julai Pili mwaka huu.
-
Burkina Faso yakanusha ripoti ya HRW, yasema haina mashiko
Apr 29, 2024 02:36Serikali ya Burkina Faso imekanusha vikali na kulaani tuhuma ilizosema hazina msingi zilizotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch ambalo limelituhumu jeshi la serikali ya nchi hiyo kuwa lilihusika na mauaji ya mwezi Februari mwaka huu 2024 katika vijiji vya Nodin na Soro kaskazini mwa nchi hiyo.
-
HRW: Jeshi la Burkina Faso limewauwa kiholela raia 223
Apr 26, 2024 03:07Jeshi la Burkina Faso limewauwa kiholela raia 223, wakiwemo watoto wachanga kadhaa na watoto wengine wengi, katika mashambulizi dhidi ya vijiji viwili vinavyotuhumiwa kushirikiana na wanamgambo wenye silaha. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch iliyotolewa jana Alhamisi.
-
Mali, Niger na Burkina Faso zaunda muungano wa kijeshi
Mar 08, 2024 07:22Mali, Niger na Burkina Faso zimetangaza habari ya kuunda kikosi cha pamoja cha jeshi kitakachosaidia kukabiliana na utovu wa usalama uliosababishwa na harakati za makundi ya kigaidi katika nchi hizo za Afrika Magharibi.
-
Mwendesha mashtaka wa Burkina Faso: Watu 170 waliuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji vitatu
Mar 04, 2024 02:29Mwendesha Mashtaka wa serikali ya Burkina Faso jana Jumapili alieleza kuwa watu takriban watu 170 waliuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji vitatu kaskazini mwa nchi hiyo wiki moja iliyopita.
-
Waislamu wakosoa kutoakisiwa mauaji ya makumi msikitini Burkina Faso
Feb 27, 2024 07:28Makumi ya waumini wa Kiislamu waliuawa katika shambulizi dhidi ya msikiti nchini Burkina Faso, siku ambayo watu 15 waliuawa pia katika hujuma nyingine dhidi ya kanisa nchini humo.
-
Mali, Burkina Faso na Niger zajiondoa kwenye jumuiya ya ECOWAS
Jan 29, 2024 03:03Tawala za kijeshi katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger zimetangaza kuyaondoa 'mara moja' mataifa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
-
Baraza la Kijeshi Burkina Faso lazima jaribio la mapinduzi
Sep 28, 2023 07:47Baraza la kijeshi nchini Burkina Faso limetangaza kwamba, vikosi vya usalama na idara za ujasusi zilizima jaribio la mapinduzi Jumanne iliyopita.
-
Burkina Faso yalifungia jarida la Kifaransa kwa kujaribu kulifanyia dharau jeshi
Sep 26, 2023 07:35Watawala wa kijeshi wa Burkina Faso wameagiza kusitishwa usambazaji wa jarida linalochapishwa kwa lugha ya Kifaransa la "Jeune Afrique" likituhumiwa kuwa limekuwa likijaribu kushusha hadhi ya jeshi la nchi hiyo.
-
Iran yalaani shambulio la kigaidi lililoua makumi ya watu Burkina Faso
Sep 08, 2023 07:33Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali shambulio la kigaidi lililouwa makumi ya watu nchini Burkina Faso.