-
Mafuriko Kenya yauwa watu 228
May 05, 2024 23:39Idadi ya walioaga dunia kutokana na mafuriko yaliyokumba Kenya imeongezeka hadi 228 huku mamlaka husika zikiendelea kukabiliana na tishio la kimbunga Hidaya.
-
Mkuu wa Majeshi na makamanda tisa waandamizi wa Kenya wafariki katika ajali ya helikopta
Apr 19, 2024 01:13Kenya inaomboleza kifo cha Mkuu wa Majeshi (KDF), Jenerali Francis Omondi Ogolla ambaye ameaga dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana Alkhamisi katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa Kaunti ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.
-
Utafiti wafichua: Wanawake Kenya wanageuzwa tasa mahospitalini bila idhini yao
Apr 09, 2024 07:42Ripoti mpya iliyotolewa nchini Kenya imebaini kuwa wanawake wanaotafuta huduma za matibabu ya uzazi nchini humo wanafanyiwa ukaguzi wa sehemu za siri, kukatizwa uwezo wa kupata mimba na kufanyiwa upasuaji usiohitajika wanapojifungua, bila idhini yao.
-
Kenya yajipanga kununua silaha mpya za kisasa za kivita kukabiliana na ongezeko la uhalifu
Apr 07, 2024 03:32Serikali ya Kenya imetangaza kuwa imo mbioni kununua silaha mpya za kisasa za kivita ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu nchini humo.
-
Seneti ya Kenya: Watuhuniwa wa mbolea feki wafunguliwe mashtaka
Apr 01, 2024 07:10Maseneta wa Kenya wametaka maafisa wa serikali walioruhusu mbolea feki kuingia nchini humo na katika mabohari ya Bodi la Nafaka na Mazao (NCPB) wafikishwe mahakamani.
-
Familia Kenya zaanza kukabidhiwa miili ya wahanga wa Shakahola
Mar 27, 2024 04:09Serikali ya Kenya imeanza kukabidhi miili ya watu waliofariki dunia kutokana na njaa katika msitu wa Shakahola pwani ya nchi hiyo, baada ya kuagizwa na mchungaji mwenye misimamo ya kufurutu ada, Paul McKenzie kufunga hadi kufa ili eti wakakutane na Yesu (Nabi Isa AS).
-
Mgomo wa madaktari nchini Kenya umeingia wiki ya pili huku huduma za dharura zikisitishwa
Mar 22, 2024 03:28Madaktari nchini Kenya wamesitisha kutoa huduma za dharura katika hospitali za serikali na hivyo kuutumbukiza mfumo wa afya katika mgogoro mkubwa zaidi huku mgomo wa kitaifa wa madaktari ukiingia wiki ya pili jana Alhamisi.
-
Mashirika 16 ya Kiirani katika maonyesho ya afya Kenya
Mar 17, 2024 07:40Mashirika 16 ya ubunifu wa utaalamu ya Iran yanashiriki katika duru ya 24 la Maonyesho ya Sekta ya Afya nchini Kenya, yaliyopangwa kufanyika Nairobi kuanzia tarehe 17 hadi 19 mwezi Aprili mwaka huu.
-
Mgomo wa nchi nzima wa madaktari Kenya waacha wagonjwa wakitangatanga, utoaji huduma wakwama
Mar 15, 2024 04:11Madaktari kote nchini Kenya wamewaacha wagonjwa wakitangatanga baada ya kugoma kuhudumu katika hospitali za umma jana Alkhamisi, licha ya agizo la Mahakama la kuzuia mgomo wa kitaifa wa madaktari hao.
-
Kenya yaakhirisha mpango wa kutuma askari polisi Haiti
Mar 13, 2024 04:14Kenya imetangaza habari ya kuakhirisha mpango wake wa kutuma kikosi cha askari polisi 1,000 nchini Haiti, kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini, Ariel Henry.