Jun 25, 2024 07:44 UTC
  • Kenya yaruhusu kufanyika maandamano kwa masharti

Kithure Kindiki Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya amewataka vijana wanaoandamana kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 kuimarisha amani na usalama, kutobeba aina yoyote ya silaha kutakiwa kuondoka katika maeneo ya mikusanyiko ifikapo saa kumi na mbili jioni.

Serikali ya Kenya imewatadharisha wanaopanga kushiriki maandamanoni kwamba wanapasa kufuata utaritibu wa ksisheria ikiwemo kuheshimu mali na biashara za raia. 

Waziri Kindiki amesema katika taarifa yake kuwa, kwa vyovyote vile utawala wa sheria na utulivu wa umma ni mambo yanayopasa kudumishwa na wote." 

Kithure Kindiki, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya 

Kufikia saa mbili asubuhi leo polisi walikuwa tayari wameshika doria katika barabara kadhaa za kati kati ya jiji la Nairobi ambako kulitazamiwa kuwa kitovu cha maandamano hayo, huku sehemu ya mji ukifungwa hasa kuelekea maeneo ya bunge.

Wasafiri pia walitatizika alfajiri kwani baadhi ya barabara zilionekana wazi kabisa kwa upungufu wa magari na mabasi ya umma kwa hofu ya maandamano hayo.

Vijana waliotambulika kama Gen Z wamekuwa wakifanya maandamano kwa siku kadhaa sasa nchini Kenya wakipingwa Mswada wa Fedha wa 2024 ambao umetajwa kuwa unawazidishia tu mzigo raia. 

Wakati huo huo Rais William Ruto amesema kuwa  yuko tayari kuwashirikisha vijana katika juhudi za kulitafutia ufumbuzi suala la muswada wa fedha nchini humo. Rais Ruto amebainisha hayo baada ya kushuhudiwa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa siku kadhaa sasa.

 

Tags