Jun 29, 2024 02:25 UTC
  • Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel: Israel inapaswa kukomesha mauaji ya kimbari ya watu wa Palestina

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel wa Uingereza amesema kuwa, amani kwa Wapalestina inawezekana tu iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utakomesha siasa za ubaguzi wa rangi na mauaji ya kimbari.

Mairead Maguire, alianzisha harakati ya Peace People kwa ajili ya amani ya watu wa Ireland ya Kaskazini, ambayo imekuwa sauti yenye nguvu ya kutetea haki katika maeneo mengine yenye migogoro duniani kote, ikiwa ni pamoja na Palestina.

Mwanaharakati huyo wa kutetea haki za binadamu tayari amefukuzwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel za Palestina mara tatu kwa nyakati tofauti akijaribu kufikisha misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina.

Mairead Maguire ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1976 amesema: "Amani haiwezi kupatikana kwa msingi wa mauaji ya kimbari, na hili linatokea kwa njia ya kusikitisha kwa watu wa Palestina."

Mwanaharakati huyu wa amani wa Ulaya amethibitisha kwamba, alitembelea Palestina mara nyingi na ameshtushwa na mateso makubwa wanayopata Wapalestina kutoka kwa Waisraeli, na kuongeza kuwa, Israel ni serikali ya kibaguzi ambayo inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wanaofanya jitihada za kukomboa nchi yao. 

Mairead Maguire akiwa Gaza

Mwanaharakati huyo wa kutetea haki za binadamu amekosoa ushiriki wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi katika uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa, Marekani imewakatisha tamaa walimwengu kwa sababu inafadhili mauaji ya kimbari na inatayarisha silaha kwa ajili ya jinai kubwa huko Palestina.

Tags