Jun 30, 2024 07:41 UTC
  • Chile yajiunga na malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni

Chile imetangaza kujiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai ya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, serikali ya Chile imetangaza kujiunga na malalamiko hayo leo, kwa nia ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaoshambuliwa na kuuawa kila siku huko mjini Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Tarehe 29 Disemba 2023,  Afrika Kusini iliwasilisha malalamiko dhidi ya utawala wa Kizayuni kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa madai ya kukiuka Makubaliano ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari, ambayo yalipitishwa mwaka 1948.

Baada ya hapo, nchi kadhaa zikiwemo Palestina, Uturuki, Libya, Mexico, Nicaragua na Colombia zilijiunga na malalamiko hayo katika kuwaunga mkono Wapalestina madhulumu wasio na hatia huko Ukanda wa Gaza.

Chile pia ilijiunga na malalamiko ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni

Mahakama ya ICJ imeutaka utawala wa Kizayuni kusimamisha hujuma dhidi ya mji wa Rafah ulioko kusini mwa Gaza na kuchukua hatua za kuzuia kutokea mauaji ya halaiki na kuboresha hali ya kibinadamu huko Gaza.

Hata hivyo, Tel Aviv inaendeleza vita hivyo wakati Baraza la Usalama limetoa azimio la kutaka kusitishwa mara moja kwa vita vinavyoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel huko Ukanda wa Gaza. Idadi ya mashahidi wa vita huko Gaza imefikia watu elfu 37, 834 tangu Oktoba 7, 2023, mwaka jana.

Aidha maelfu ya watu bado hawajulikani walipo chini ya vifusi, na vikosi vya kutoa misaada haviwezi kuwafikia kutokana na  vizuizi vilivyowekwa  na utawala wa Kizayuni huko Palestina, na vita vinavyoendelea, na ukosefu wa vifaa pia.

Tags